HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 16, 2018

MALEZI BORA NI MSINGI KATIKA UJENZI WA FAMILIA IMARA NA TAIFA IMARA

 Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota akiwasisitiza wazazi kuchangia ujenzi wa famila na taifa kwa kuwapa  malezi bora watoto  wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi Magreth Mussai akizungumzia umuhimu wa malezi bora katika familia na wajibu wa wazazi katika kutoa malezi hayo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota( wa pili kushoto) akipokea bango la wadau kutoka nchi za ulaya wanaounga mkono jitihada za Serikali ya Tanzania kupinga ndoa za utotoni wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.  
Nesi akimchoma mtoto wa Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Vanessa Makota Chanjo ya Saratani ya Shingo ya Kizazi katika uzinduzi wa chanjo hiyo Wilayani Kondoa wakati wa maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani iliyofanyika Wilayani humo.  
Wanafunzi na Wananchi wa Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma wakifuatilia mambo mbalimbali katika Siku ya Familia Duniani yaliyokuwa yakifanyika katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma. Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW



Malezi bora katika familia imesemeka ni ndio msingi wa malezi kwa watoto katika jamii yetu hivyo wazazi wanapaswa kuzingatia kutoa malezi bora kwa watoto ndani ya familia na jamii kwa ujumla ili kuwa na taifa lenye uchu wa kujiletea maendeleo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mhe.Vaileth Makota  wakati akisoma Hotuba ya Wziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto katika  maadhimisho ya Siku ya Familia Duniani yaliyofanyika Wilayani Kondoa katika Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Vaileth Makota amesema kuwa wazazi wanawajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora na katika maadili mazuri ili kujenga taifa bora lenye watoto wanaojitambua, wanaojithamini, na wenye maadili mema ili kulitumikia Taifa.

Ameongeza kuwa wazazi wanatakiwa kuwa walimu kwa matendo yao kwa watoto kwani watoto wanaiga yale ambayo wazazi wanafanya hivyo tabia na mienendo yao ni kati ya vitu ambavyo vitasababisha malezi mabaya au bora kwa watoto na jamii kwa ujumla.

Amesisitiza kuwa wazazi wana wajibu wa kuwalea watoto katika malezi bora ili kujenga utu, uzalendo na upendo kwa watoto na jamii kwani malezi katika familia ni msingi katika ujenzi wa taifa linalozingatia uzalendo, maadili mema, utu na uwajibikaji katika maendeleo yao na taifa.

“Tuzingatie katika kutoa malezi bora kwa watoto wetu ili tujenge taifa bora lenye maadili mema kwa maendeleo ya taifa” alisisitiza Mhe. Vaileth

Kwa  upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mtoto Bibi. Magreth Mussai amesisitiza watoto na vijana kuwa na maadili kwa wazazi na wanajamii ili kujenga taifa lenye maadili na upendo.

Siku ya Familia Duniani inaadhimishwa kila Mei 15, 2018 na kwa mwaka huu inaadhimishwa ikienda na kaulimbiu isemayo “Malezi Jumuishi: Msingi wa Uzalendo, Utu na Maadili ya Familia na Taifa’’.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad