HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 22 May 2018

TULIA TRUST YAWAPELEKA BUJORA DANCE GROUP KUWAKILISHA NCHI NGOMA ZA ASILI NCHINI INDIA

Mwanakikundi wa Bujora Deogratius Willium akizungumza kabla ya kuanza safari ya kuelekea nchini India kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kucheza baada ya kuibuka washindi katika mashindano ya Tulia Traditional Dance Festival mwaka jana yaliyo chini ya Naibu Spika Dkt Tulia Ackson.

Na Zainab Nyamka, Blogu ya jamii

WASHINDI wa Tulia Traditiona Dance Festistal 2017 chini ya Taaisisi ya Tulia Trust Bujora Dance Group la Mkoa Mwanza leo  wameelekea nchini India kushiriki mashindano ya ngoma ya asili yatakayofanyika tarehe 25 na 26 wiki hii.

Akizungumza na vyombo vya habari mmoja wa wanakikundi hao Deogratius Willium ameeleza kuwa walishinda katika mashindano ya Tulia dance mwaka jana na kwa sasa wanaelekea India katika mashindano hayo ya ngoma za asili.

Aidha ameeleza kuwa wana uzoefu na wamejiandaa na wanajiamini, na kuwaomba watanzania wawaombee ili waweze kurudi na ushindi.

Pia Veronika  Sombi mshiriki wa kikundi hicho ameeleza kuwa ameeleza kuwa walishinda kwa kishindo Mbeya kwa kuibuka nafasi ya kwanza kati ya vikundi 81, hivyo ushindi lazima urudi nyumbani.

Pia wamemshukuru Dk. Tulia kwa kuanzisha mashindano hayo kwani kama vijana wamepata fursa ya kutangaza utamaduni wa mtanzania sambamba na kutembea katika nchi nyingi duniani kama Sweden na Korea.

Mashindano haya ya kulinda utamaduni yalianza mapema mwaka 2016 huko Tukuyu Mkoani Mbeya chini ya Dkt. Tulia Ackson ambaye ni naibu spika wa Bunge la Jamuhuri wa muungano wa Tanzania, pia ni muasisi wa mashindano hayo. 

Washindi wa mashindano hayo hunufaika kwa namna mbalimbali kama vile kueneza utamaduni nje ya nchi na kupata mafunzo katika vyuo vya sanaa hasa Bagamoyo ambapo washindi wa mwaka 2016 waliendeleza ujuzi  katika chuo hicho cha sanaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad