HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 16, 2018

BALOZI KIDATA AMUAGA MAKAMU WA RAIS LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kuzungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada, Balozi Alphayo Kidata, ofisini kwake Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Balozi Kidata ambaye aliapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Canada tarehe 10, Mei 2018 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Joseph Pombe Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Balozi Kidata alifika leo kuona Makamu wa Rais na kumuaga rasmi tayari kwa kwenda kulitumikia Taifa kwenye kituo chake kipya cha kazi nchini Canada. 

Makamu wa Rais, Mhe. Samia amempongeza na kumtakia kazi njema ambapo alimtaka kwenda kufanya yale nchi imeelekeza haswa katika kuhakikisha Tanzania inakuwa nchi ya Uchumi wa Viwanda.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais) 
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Balozi mpya wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata aliyefika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja  na Balozi wa Tanzania nchini Canada Mhe. Alphayo Kidata mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuaga kabla ya kwenda kwenye kituo chake kipya cha kazi. 
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad