HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 5, 2018

WAZAZI CCM PWANI WATOA DAMU,WACHANGIA UJENZI SHULE YA MSINGI AMANI

Na Elisa Shunda, Bagamoyo
JUMUIYA ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani imeadhimisha siku ya wazazi kwa mkoa huo kwa kuchangia kutoa damu chupa 120 na kutoa mifuko 50 ya simenti,mabati 100 na matofali 200 vyenye thamani ya Shilingi Milioni Tatu na Laki Saba na Hamsini kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi Amani Voda iliyopo Mbwewe wilayani Bagamoyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa mkoa na wilaya waliohudhuria katika maadhimisho hayo wamesema kuwa jukumu kubwa walilonalo jumuiya ya wazazi ni kuhakikisha wanajitahidi kwa hali na mali kuhakikisha wanatumia nguvu na mali kusaidia katika elimu,mazingira na afya ambayo yanagusa jamii ya watu wengi.

Akizungumza katika maadhimisho hayo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno alisema kuwa muda haumsubiri mtu na kuwasisitiza wawakilishi wa majimbo na kata wa chama hicho kutekeleza ahadi walizoahidi kuzitoa kwa wananchi wao wahakikishe wanazitekeleza wao kama viongozi hawatakubali chama kije kiadhibiwe katika chaguzi zijazo kwa ajili ya uzembe wa mwakilishi wa wananchi hao.

“ndugu zangu wawakilishi mliochaguliwa na wananchi kuwawakilisha bungeni na kwenye vikao vya halmashauri ni muda muafaka sasa wa kuhakikisha kabla ya uchaguzi mkuu haujafika hakikisheni mnatatua changamoto na kero za wananchi wenu mnaowawakilisha,haiwezekani chama chetu kiadhibiwe na wananchi ambao ndiyo wapiga kura kwa uzembe wa kutowajibika ipasavyo kwa watu hawa waliokuchagua hata nyie wenyeviti wa serikali za mitaa wahudumieni kwa haki wananchi wenu kama inavyotakiwa bila ya upendeleo” Alisema Maneno.

Aidha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka,amewakumbusha viongozi wa jumuiya hiyo kuwatumikia wananchi na wanachama wa chama hicho kwa kuwatumikia katika misingi waliyojiwekea katika sekta ya elimu,mazingira pamoja na masuala ya afya kwa kusaidia kwa hali na mali lakini pia ametoa rai kwa wazazi kuhakikisha vijana majumbani wanakuwa na maadili kwa kuwafunda watoto wa kiume kutovaa herein masikioni,kuvaa suruali nusu ya makalio na kunyoa kiduku.

Hata hivyo Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani,Gama J. Gama aliwausia wakazi wa Mbwewe kujitolea kwa hali na mali katika ushiriki wa michango ya maendeleo ya kijiji au kata kwa kuamua kujitolea pasipo kulazimishwa na kuacha kusubiri wahisani kwa kuwa ujenzi wa darasa ulianzishwa na jumuiya hiyo ya wazazi miaka mine ilibidi wao pia wajichangishe na kuwasisitiza kuonyesha mfano.

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanajumuiya na wanchama wa Chama Cha Mapinduzi Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo,Abubakar Mlawa,alisema kuwa wamefarijika kuona maadhimisho ya siku ya wazazi kimkoa imefanyika katika wilaya yao lakini pia wamefurahi pia kuona ahadi ya ukamilishaji wa ujenzi wa darasa ndani ya shule ya msingi ya Amani Voda umekamilika kwa kutoa mifuko ya simenti 50,mabati 100 na matofali 200 na kuahidi kufanyia kazi changamoto zote zilizojitokeza.

Aidha kwa niaba ya wenyeviti wa wilaya zingine za Mkoa wa Pwani,Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda alisema kuwa wamepokea maagizo yote yaliyotolewa na viongozi wa mkoa na kuahidi kuyafanyia kazi kuhakikisha jumuiya ya wazazi inakuwa imeimalika katika kutekeleza majukumu yake.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno akimkabidhi Mabati 100,Mfuko wa Simenti 50 na Matofali 200,Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (kulia) iliyotolewa na wadau mbalimbali wa elimu kwa ajili ya ujenzi wa darasa la Shule ya Msingi ya Amani Voda iliyopo Mbwewe. Picha zote na Elisa Shunda.
 Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani,Ramadhan Maneno (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Mkoa wa Pwani,Jackson Kituka (katikati) na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Bagamoyo.
 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani,Gama J Gama akizungumza katika mkutano huo.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,Saidy Omary Zingatimbu akizungumza katika mkutano huo.











 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chalinze,Saidy Omary Zingatimbu akitoa damu katika kituo cha afya cha Lugoba.



 Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM Mkoa wa Pwani,Gama J Gama na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa CCM wa Wilaya ya Kibaha Mjini,Edwin Shunda wakipanda miti katika eneo la Kituo cha Afya cha Lugoba.






No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad