HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 5, 2018

WANAFUNZI VYUO VIKUU WASHAURIWA KUTUMIA VYEMA MAWAZO YAO

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
BENKI ya dunia kupitia mradi wake wa kuinua uchumi wa nchi mbalimbali Afrika April 4 umewatangaza washindi wake katika shindano la Blog4Dev2017 lililofanyika mwaka jana likiwa na malengo ya kutafuta vijana walio na mawazo thabiti ambayo yatasaidia katika kutatua tatizo la ajira nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam katika utoaji wa tuzo kwa washindi hao mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia nchini bi Bella Bird  ameeleza kuwa wamewapata washindi hao kutokana na uandishi mzuri wa insha bora katika kuangalia namna ya kutatua matatizo ya ajira nchini katika maeneo ya kilimo na teknolojia.

Bi Bella ameeleza kuwa washindi watawasilisha mawazo yao katika mjadala ulioandaliwa huko Washngton Dc mapema wiki ijayo.

Aidan Nzumi mmoja wa washindi wa shindano hilo ameeleza kuwa amefurahi kuwa mmoja wa vijana wataobadilisha maisha ya vijana wengi  na ameeleza kuwa kilimo ni kizuri katika kujiajiri  licha ya kuwa na changamoto katika hali ya hewa na taarifa hasa za masoko na mikopo pia amewataka  vijana walio shule na vyuo watumie mawazo yao katika kubadilisha maisha yao na ya vijana wengine.

Naye Michael Mollel mshiriki wa shindano hilo ameishukuru benki ya dunia kwa kupokea mawazo yao na kuyafanyia kazi ambazo na kwa namna moja au nyingine zitatoa ajira.
 Bella Bird Mkurugenzi mkazi wa benki ya dunia akiwa na washindi wa Blog4Dev2017 katika picha ya pamoja.
Baadhi ya washiriki na wanafunzi wa vyuo mbalimbali waliohudhuria hafla ya utoaji wa tuzo kwa washindi hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad