HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 12 April 2018

WADAU WA UKANDA WA KATI WATEMBELEA BANDARI DAR ES SALAAM

Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) wametembelea bandari ya Dar es Salaam ili kuona namna inavyoendesha shughuli zake pamoja na kupatiwa taarifa ya mipango iliyopo ya kuboresha zaidi huduma zinazotolewa bandarini hapo.
Akizungumzia ziara hiyo, Katibu Mtendaji wa Ukanda wa Kati, Kepteni Dukundane Dieudonne alisema wametembelea bandari baada ya kufanya kikao cha siku mbili na kupokea ripoti ambayo inaelezea utendaji kazi wa bandari hyo ambayo iliwarishidha hivyo wakaona ni vyema kufika bandarini ili kuona utendaji wake.
“Tuna furaha kukaribishwa katika bandari ya Dar es Salaam, tuna furaha ya kuona mambo mengi ambayo bandari inafanya ili kutoa huduma kamilifu kwa wadau wote wa Ukanda wa Kati,” alisema Dukundane na kuongeza.
“Tunaipongeza TPA kwa mafanikio mazuri na tumeona mzigo umeongezeka katika bandari hii, wale waliokuwa wanasema wateja wamehama hiyo sio kweli tumeona wadau wengi wamerudi bandari ya Dar es Salaam.”
Naye Mkurugenzi wa Wadau wa Ukanda wa Kati, Desire Hishamunda aliipongeza hatua zinazochukuliwa na TPA ili kuboresha huduma bandarini hapo na kutaka hatua zaidi ziendelee kuchukuliwa ikiwa na pamoja na kuongeza kasi ya utoaji huduma ili meli ziwe zinashusha mzigo kwa haraka na usafirishwe kwenda kwenye nchi zinazopitisha mizigo hapa nchini.
Wadau wa Ukanda wa Kati waliotembelea bandari ya Dar ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Rwanda na Uganda.
 Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya(kushoto) akisalimiana na Katibu Mtendaji wa Ukanda wa Kati, Kepteni Dukundane Dieudonne(katikati) mara baada ya kuwasili bandari ya Jijini Dar Es Salaam pamoja na  wadau wa Ukanda wa Kati ili kujionea ufanisi wa bandari hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akizungumza jambo na ujumbe wa wadau wa Ukanda wa Kati uliotembelea bandari ya Dar es Salaam walipotembelea mabanda ya maonesho yao.
Afisa wa TPA akitoa maelezo kuhusu wiki ya TPA kwa ujumbe wa wadau wa Ukanda wa Kati uliotembelea bandari ya Dar es Salaam
Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya akitolea ufafanuzi kuhusu TPA upanuzi bandali ili kuboresha huduma ambazo zinatolewa bandarini hapo kwa wadau wa Ukanda wa Kati waliotembea bandari hiyo.
 Kaimu Mkurugenzi Masomo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari nchini (TPA), Lydia Mallya  akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) kutembelea banadari ya Dar es Salaam ili kuona namna inaendesha shughuli zake pamoja na kupatiwa taarifa mipango iliyopo ya kuboresha zaidi huduma zinazotolea banadarini hapo.
Katibu Mtendaji wa Ukanda wa Kati, Kepteni Dukundane Dieudonne akizungumza na waandishi wa habari mara baada Wadau wa Ukanda wa Kati (Central Corridor) kutembelea banadari ya Dar es Salaam na kujionea ufanisi wa bandari hiyo
Mkurugenzi wa Wadau wa Ukanda wa Kati, Desire Hishamunda akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kujionea hatua zilizochukuliwa na TPA ili kuongeza kasi ya utoaji huduma ili meli ziwe zinashusha mzigo kwa haraka na usafirishwe kwenda kwenye nchi zinazopitisha mizigo hapa nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad