HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 9, 2018

TPDC najitihada za kulihakikishia Taifa gesi ya kutosha

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) akiwammiliki wa leseni za vitalu vya gesi na mafuta nchini kwa kushirikiana na mkandarasi, kampuni ya Dodsal wanaendelea kufanya utafiti (ukusanyaji wa takwimu za mitetemo “2D seismic data” utafiti unahusisha eneo lenye urefu wa takribani km 1287) zaidi wa gesiasilia katika Kitalu cha Ruvu kilichopo Mkoa wa Pwani na baadhi ya maeneo ya Dar es salaam kwa lengo la kuhakikisha kuwa Tanzania inapata gesi asilia au mafuta ya kutosha itakayojenga uchum iimara wa viwanda.

Akielezea umuhimu wa utafiti huo, Simon Kimario ambaye ni Mjiofizikia kutoka TPDC amesema kuwa lengo kuu la utafiti huo nimuendelezo wa utafiti wa mafuta na gesi unaofanywa na mwekezaji Dodsal Hydrocarbons akishirikiana na TPDC katika kitalu cha Ruvu ilikuwezesha kugundua gesi asilia nyingi zaidi na pengine mafuta ilikuhakikisha Taifa linakuwa na chanzo imara cha nishati ambacho kitalisaidia taifa katika kujenga uchumi wa viwanda.
Ramani inayoonyesha kitalu cha utafiti cha Ruvu

“Tayari hatua kadhaa zimeishafanyika kama vile; uandaaji wa ramani ya kiutafiti ambayo kazi yake nikuonyesha eneo la kitalu na maeneo muhimu ya kufanyia utafiti, ambapo kunapelekea kwenye hatua nyingine ya kwenda kwenye eneo halisi na kubaini mistaria ambayo taarifa za mitetemo zitachukuliwa, hatua ambayo itanguliwa na zoezi la kupata vibali na kuelimisha wananchi kuhusu namna zoezi zima na ushirikishwaji wa wananchi utakavyofanyika.”

Akiogelea hatua zinazoendelea sasa hivi ndugu kimario anaeleza kuwa shughuli zinazoendelea katika maeneo tofauti tofauti kwa sasa ni pamoja na usafishaji njia au mistari, kuchimba mashimo ya kina kifupi mita 7, 10 au 15 kutegemea na jiolojia ya eneo kwa ajili ya kuweka baruti (vyanzo vya mitetemo ) pamoja na kuweka mitambo maalum ya kuchukulia taarifa za mitetemo(seismic data).
Mtambo wa kuchoronga mashimo ya kuwekea baruti ukiwa kazini. Mtambo huu huchimba mashimo yenye urefu tofauti kati ya mita 7 hadi 15, kwaajili ya kufukia baruti ambazo zinapolipuliwa ndipo taarifa za miamba chini hupatikana baadae kuchakatwa na kutafsiriwa kitaalam ilikujua sehemu ya kuchimba kisima cha utafiti.

Aidha anaeleza kuwa, “Yapo maeneo mengine ambayo yamefikia kwenye hatua ya kubainisha maeneo maalum yatakayowekewa baruti pamoja na vifaa vya kunakili au kunasa taarifa za mitetemo, yapo maeneo ambayo tayari zoezi hili limeshafanyika na tayari hatua ya kulipua baruti na kunakili taarifa za mitetemo limekwishaanza kufanyika”.

Simon amethibitisha kuwa hadi sasa takribani mashimo yaliyopo kwenye misatri yenye urefu wa km 311 yameishasimikwa au kujazwa na baruti na mistari ya kijiofizikia yenye urefu wa Kilomita 116.9 kati ya 1287 imeshachukuliwa taarifa za kijiofizikia na kuendelea kufanyiwa uchambuzi wa awali.
Mmoja wa wataalam wa milipuko akipima urefu wa shimo kama limekidhi mahitaji ya kitaalam kabla ya kusimika/kujaza baruti ndani ya shimo.

Aidha akiongolea suala la vibali na fidia kwa wananchi ambao mazao yao yameathirika na yatakayoathirika na zoezi la uchukuaji wa taarifa za mitetemo, Mohamed Ally ambaye ni Msimamzi wa Vibali kutoka kampuni ya Envision Consulting Ltd ameeleza kuwa kumekuwa na ushirikiano mkubwa sana kutoka TPDC haswa panapohitajika vibali kutoka katika mamlaka mbalimbali za serikali na hivyo kumefanya kazi yao kuwa rahisi na yenye mafanikio.

Akiongolea suala la fidia, Mohamed anabainisha kuwa “pamoja na kuwa na mtathamini wamekuwa wakifanya kazi hiyo kwa kushirikiana na viongozi kutoka ofisi za Kata, Wilaya, Mikoa pamoja Mthamini Mkuu wa wa Serikali na hivyo kufanya zoezi zima la uthamini na ulipaji fidia kufanyika kwa mafanikio makubwa na kupunguza migogoro na wananchi”.
Moja ya baruti zinazofukiwa chini ikiwa kwenye maandalizi ya kufukiwa kwenye shimo maalum kwa ajili ya kulipuliwa.

Pamoja na utafiti unaofanyika katika kitalu cha Ruvu, TPDC linaendelea na maandalizi ya utafiti katika maeneo mbalimbali nchini kama vile vitalu vya; Eyasi-Wemberi, Songo Songo Magharibi, Mnazi Bay kaskazini pamona na Vitalu vya 41B/41C.
Moja ya kitafaa maalumu (AVO) ya kunakili taarifa za mitetemo za kijiofizikia kikiwa kimesimikwa ardhini tayari kusubiri mitego ya baruti kulipuliwa ili kupata taarifa za mitetemo. Mtambo huu hutumika ili kupata taarifa za mitetemo zenye taswira ya pande mbili “2D”.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad