HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 3, 2018

SUKOS YATOA ELIMU KUKABILI MAJANGA KWA WANAFUNZI SHULE ZA SEKONDARI

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
IMEELEZWA ipo haja ya kutoa mafunzo ya elimu ya majanga na maafa kwa wanafunzi kwani husaidia kuwa mabalozi wazuri kwenye jamii kuelezea namna ya kuchukua tahadhari mapema.

Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam na Mkurugezi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu wakati Taasisi ya Sukos kwa kushirikiana na Vodacom Foundation kutoa vifaa mbalimbali vya kujikikinga na majenga.

Ambapo amesema kuwa vifaa vya kutumia wakati majanga yanatokea ni muhumu sana na kuongeza SUKOS na Vodacom Foundation zimeona mbali zaidi katika kutoa vifaa vya kutumia pale majanga yanapotokea hasa katika shule ambapo zimekuwa zikikumbwa na majanga ya moto.

Amesema kuwa Serikali inatambua mchango wa wadau katika kujitoa kwa jamii kwa ajili ya kutoa elimu ya majanga na namna ya kuweza kukabili.

Kwa upande wake Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos, Kamishina Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova amesema majanga yanapotokea lazima watu wawe na elimu ya kupambana ili madhara yasitokee au kupunguza madhara.

Amesema Sukos imekuwa mstari wa mbele kutoa elimu kwa wananchi wajihami na majanga kwa kukabiliana na vifaa vya majanga hayo kutokana na elimu walioipata.

Wakati huohuo Meneja wa Vodacom Foundation,  Sandra Oswald amesema Vodacom Foundation imeona kuna umuhimu wa kutoa vifaa vya kukabiliana na majanga katika taasisi ya Sukos kufikisha katika shule. Shule za sekondari zilizonufaika kwa elimu na vifaa, Mtakuja , Makumbusho , Kinyerezi  pamoja Kambangwa.
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya kupambana na majanga mbalimbali katika shule za sekondari za jijini Dar es Salaam.
 Mwasisi na Mkurugenzi Mtendaji wa Sukos, Kamishina Mstaafu wa Jeshi la Polisi, Suleiman Kova akizungumza na wanafunzi kuhusiana na majanga mbalimbali yanayotokea na kushindwa kuyakabili kutokana na kukosa elimu ya majanga pamoja na elimu ya kutumia vifaa mbalimbali katika kujiokoa katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam.
 Meneja wa Vodacom Foundation, Sandra Oswald akipokea chati cha kutambua mchango Vodacom Foundation katika kutoa vifaa vya kukabiliana majanga mbalimbali ikiwemo Moto katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam.
 Afisa Habari wa Jeshi la Zimamoto, Amani Hassan akiwafundisha wanafunzi jinsi ya kutumia Fire Extyingusher wakati moto ukiwa unatokea katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam
 Mkurugenzi Msaidizi (Mipango na Tafiti) Idara ya Uratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bashiru Taratibu akimkabidhi  Fire Extinguisher mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Makumbusho, Sumaiya  Saidi katika hafla iliyofanyika shule ya Sekondari Mtakuja jijini Dar es Salaam 
Sehemu vifaa vilivyotolewa na Vodacom kwa ajili ya SUKOS kugawa katika shule za Sekondari Nne za jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad