HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, 10 April 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania kushirikishwa katika Tuzo za The African Prestigious Awards


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (watatu kushoto) akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa jana jijini Dar es Salaam anayetarajia kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kushoto ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.


Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (wapili kushoto) akimkabidhi Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa tiketi ya ndege jana jijini Dar es Salaam kwa ajili ya safari yake ya kwenda nchini Ghana mapema wiki hii katika tuzo za The African Prestigious Awards ambapo amechaguliwa kuwania kipengele cha Msanii Bora wa Kike Afrika,kutoka kulia wapili ni Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Sanaa Bibi. Leah Kihimbi na wa kwanza kulia ni Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa Tanzania Bw.Godfrey Mngereza.


Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(wakwanza kushoto) akifafanua kwa waandishi wa habari na wadau wa sanaa (hawapo pichani) kuhusu tuzo za The Africa Prestigious Awards jana jijini Dar es Salaam zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni kwa kueleza heshima ya tuzo hizo na Tanzania imepata heshima ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli nae kuteuliwa kuwania tuzo ya kiongozi bora Afrika,wa kwanza kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe.


Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie maarufu kama Monalisa akiahidi kwa Waziri wa habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe (hayupo pichani) jana jijini Dar es Salaam katika sherehe ya kukabidhiwa bendera kuwa atarudi na tuzo hata kama yeye hatopata basi ataweza na kurudi na hata tuzo ya Msanii Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika au Tuzo ya Msanii King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika au Mpiga picha Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga picha Bora Afrika katika tuzo za The African Prestigious Awards zitakazotolewa nchini Ghana hivi karibuni,wa kwanza kulia ni Mama Mzazi wa Msanii Monalisa Bibi Suzan Lewis maarufu kama Natasha.Na Anitha Jonas – WHUSM

Utendaji uliyotukuka wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  John Pombe Magufuli na ukuwaji wa sekta ya filamu nchini ndiyo vinavochangia kuitangaza nchi yetu katika tuzo za The African Prestious Awards.

Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe alipokuwa akimkabidhi bendera msanii wa filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kwenda nchini Ghana katika tuzo hizo.

“Tanzania imepata heshima kubwa katika tuzo hizi zenye heshima kubwa katika bara la Afrika ambapo Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli ameteuliwa kuwania Tuzo ya Kiongozi Bora Afrika, napia tuna wasanii watatu ndani ya tansia ya filamu ambao ni King Majuto anayewania Tuzo ya Mchekeshaji Bora Afrika,Raymond Kigosi anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume Afrika na Monalisa mwenyewe anayewania Tuzo ya Msanii Bora wa Kike Afrika pamoja na Mpiga picha Mahiri Moiz Hussein anayewania Tuzo ya Mpiga Picha Bora Afrika,”alisema Dkt.Mwakyembe.

Akiendelea kuzungumza katika sherehe hiyo ya kukabidhi bendera Mheshimiwa Mwakyembe aliwasisitiza wasanii wanchini kuendelea kuandaa kazi zinazoonyesha ubunifu wao kwani ukuaji wa tansia ya filamu Tanzania uko mikononi mwao na si vinginevyo.

Pamoja na hayo nae Msanii wa Filamu nchini Yvonne Cherrie Maarufu kama Monalisa anayetarajia kuondoka nchini mapema wiki hii kwenda nchini Ghana kwa ajili ya Tuzo hizo aliwaahidi watanzania kuwa lazima atarudi na tuzo kwani anawawakilisha wasanii wenzake hao wawili pamoja na mpiga picha huyo aliyetajwa na pia aliishukuru serikali kwa kumpatia tiketi kwa ajili ya kufanikisha safari hiyo.

“Tuzo hizi nazichukulia kama ni heshima kubwa sana kwangu kwani kipengele ninachowania kinahusisha wasanii wakubwa katika bara la afrika kwani niko pamoja na Lupita Nyongo ambaye ni mwigizaji wa Hollywood pamoja na Jackie Apia ambaye nae anafanya vizuri hivyo hata nisipopata tuzo hii kwangu kuchaguliwa kwanza katika kipengele hicho tayari ni ushindi kulinga na uwezo wasanii wenzangu tuona shindana,”alisema Monalisa.

Kwa upande wa Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu nchini Bibi.Joyce Fissoo alisema anafurahishwa kuona sekta ya filamu ya nchini ikikua na kuleta taswira mpya katika bara la afrika ambapo wasanii watanzania nao kazi zao zinavuka mipaka na kuleta changamoto katika ushindani katika tasnia filamu Afrika.

Hata hivyo nae mama mzazi wa Monalisa Bibi.Suzan Lewis maarufu kama Natasha alieleza kufurahishwa na kazi ya filamu anayoifanya mwanaye na pia alieleza kuwa anamtakia mafanikio makubwa pamoja na kushinda tuzo hiyo.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad