HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 April 2018

NGORONGORO HEROES TUNACHOHITAJI NI USHINDI TU - NINJE

Na Zainab Nyamka,Globu ya jamii

KOCHA Mkuu wa Ngorongoro Heroes Ammy Conrad Ninje amesema wao hawataangalia ni waamuzi gani watakaochezesha mchezo huo ingawa Shirikisho la soka barani Afrika limetoa orodha ya waamuzi watakaotumika katika mchezo huo kutoka Congo Brazaville.

Kumeibuka na mjadala wa kwanini Mwamuzi wa Congo Brazzaville Fitial Charel Just Kokolo ameteuliwa kuchezesha pambano hilo, hata hivyo Ninje amesema hawatakuwa na wasiwasi kwani wanaamini haki itatendeka na kumpata mshindi kihalili.

"Sisi tunachohitaji ni fair unajua hatuwezi kupangua na pia lipo nje ya uwezo wetu, ila tunawahitaji wachezeshe kwa haki, atakayeshinda basi apate nafasi ya kusonga mbele, ukiangalia sisi na Congo DR tupo karibu kama ilivyokuwa kwa Congo Brazzaville lakini wao wapo karibu zaidi .Mimi nawatayarisha vijana wangu tukacheze mpira vizuri tujaribu kutumia nafasi zetu.

"Tusiangalie refarii, sisi wenyewe tujipange kwenda kuwa washindani na kuangalia ni mbinu gani tutazitumia ili tupate ushindi," ameeleza Ninje.

Kwa kukumbusha Ngorongoro Heroes watakuwa na kibarua kizito April 22 mwaka huu katika Uwanja wa Stade Des Martyrs uliopo katika jimbo la Kinshasa ambapo watalazimika kupata ushindi wa aina yoyote ama sare ya mabao ili kusonga mbele na kukutana na Mali.

Waamuzi wa mchezo huo wa marudiano wote wanatoka Congo Brazzaville .Muamuzi wa kati atakuwa Fitial Kokolo, waamuzi wasaidizi ni Beaudrel Ntsele Roul na Tritton Franck Audiard Diawa.
Katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 0-0 Kabwili alionesha kiwango bora kwa kuokoa hatari nyingi ambazo zilielekezwa langoni.

Hata hivyo katika michezo miwili ya kirafiki kati ya Msumbiji na Morocco kipa Aboutnalib Mshery alionesha kiwango kizuri pia.

Katika hatua nyingine kocha Ninje amesema kambi inaendelea vizuri na wamekuwa na mazoezi mazuri kwani sasa wamekuwa wakifanya mazoezi mara mbili kwa siku, wakijaribu kutatuta tatizo la ufungaji ambalo limejionesha katika michezo mitatu hadi hivi, huku ukizingatia kuwa wanahitaji kufunga bao katika mchezo wa marudiano.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad