HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 9 April 2018

MAKAMU WA RAIS ZANZIBAR ATEMBELEA BANDA LA MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA(TCAA)

Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi  ametembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA).TCAA ni miongoni mwa taasisi na kampuni zinazoshiriki mkutano wa Saba (7) wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) unaofanyika katika hoteli ya Zanzibar Beach Resort Kuanzia April 9-10, 2018. Mkutano huu unatoa fursa kwa watumiaji na watoa huduma za usafiri wa anga kuonyesha maendeleo katika sekta.
 Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa Pili Kulia o)  Akimsikiliza Mwanasheria Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Vallery Chamulungu(wa Kwanza Kushoto) alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) Yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.
  Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa pili kushoto)  alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.Wengine kutoka Kushoto ni  Waziri wa Miundombinu, Uchukuzi na Mawasiliano Zanzibar, Dr. Sira Ubwa Mamboya na Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Eng. Ladslaus Matindi.
Makamu wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa Kwanza kulia)  Akifurahia Jambo na Maafisa wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) alipotembelea banda la maonyesho la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TCAA) Katika mkutano wa Umoja wa Kampuni za Ndege Barani Afrika(AFRAA) Yanayofanyika Zanzibar Beach Resort kuanzia April 8-10, 2018.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad