HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, April 12, 2018

Kampuni ya Imports International yatoa mafunzo kwa wakazi wa na wafanyabiashara Karikoo

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Kampuni ya Imports International Tanzania imetoa mafunzo ya siku moja kuhusu jasi (gypsum) kwa wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi katika soko la Kariakoo lililopo Ilala jijini Dar es Salaam.

Akizungumza akizungumza na MMG  ,  Mtaalamu wa ujenzi wa kampuni ya Imports International Tanzania, Stanley Katabarwa amesema lengo la kutoa mafunzo hayo ni wafanyabiashara wajue aina za gypsum kutokana na sehemu ambayo inakwenda kutumika.

Amesema wafanyabiashara wengi wanauza gypsum lakini hawajui matumizi sahihi hivyo uwepo wao katika eneo hilo utasaidia wafanyabiashara hao kuuza gypsum kulingana na mahitaji ya mteja.

"Mara nyingi huwa tunakosea gypsum ya kutumia kulingana na shemu inayokwenda kutumia matokeo yake uimara ya hiyo sehemu inakuwa haipo," amesema Katabarwa na kuongeza.

"Tumeshafanya mafunzo ya aina mbili ambayo yalihusisha wadau wengine wa ujenzi na leo hapa tunalenga mafundi na watu ambao wanauza, sio kwamba wanauza bidhaa bila kuzielewa. Tunataka tu watu waelewe njia nzuri ya kutumia gypsum bora."

Aidha Katabarwa alisema kampuni yao inazo gypsum za aina zote na hivyo kwa wanaohitaji wanaweza kufika katika ofisi zao ili wanunue na kuzitumia katika ujenzi.

 Mtaalamu wa ujenzi wa kampuni ya Imports International Tanzania, Stanley Katabarwa akionesha namna ya kuweka gypsum katika nyumba ikiwa ni wiki ya kampuni hiyo kutoa elimu kwa wafanyabishara wa vifaa vya ujenzi wa Karikoo, jijini Dar es Salaam.
Wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakiangalia na namna Gypsum ilivyowekwa kwa ustadi na kampuni ya Imports International Tanzania , jijini Dar es Salaam.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad