HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 5 April 2018

Ecobank Mobile App yafikisha watumiaji milioni 4

Na Mwandishi wetu

MABADILIKO makubwa yaliyofanywa katika upatikanaji wa huduma za kibenki za ECOBANK kupitia mtandao wa kompyuta (Ecobank mobile app ) umeingiza wateja milioni tatu wapya katika kipindi cha miezi sita tangu kuzinduliwa kwake na kufanya idadi ya watumiaji wa mfumo huo kufikia milioni 4.

Mfumo huo ambao umetengenezwa kutokana na  mfumo wa awali wa huduma za kibenki kupitia mtandao umebadilisha namna ambavyo huduma za kibenki zinafanyika katika nchi za Afrika.

Nchi nyingi za Afrika zinakabiliwa na  vikwazo katika huduma za kawaida za kibenki kama kufa kwa matawi ya mabenki vijijini, ufinyu katika upatikanaji wa bidhaa mbalimbali za benki,gharama kubwa za kufanya miamala na kiwango cha fedha kinachotakiwa katika ufunguaji wa akaunti.

Mtendaji Mkuu wa  Eco Bank, Ade Ayeyemi  amesema ni mkakati wa benki hiyo kuhakikisha kwamba wanatumia mfumo wa kompyuta kutoa huduma zenye ubunifu wa hali ya juu,zenye ufanisi na gharama nafuu kwa wale ambao wapo nje ya mfumo rasmi wa uchumi.

Aidha mfumo huo umelenga kuwezesha huduma zaidi ya zile zinazotolewa na matawi ya kawaida na ATM.

Wakati watu milioni moja walitumia mfumo huu katika kipindi cha mwaka mmoja tangu uzinduzi wake, mabadiliko yaliyofanywa kuongeza huduma nyingine kumefanya watumiaji wake kuongezeka maradufu katika kipindi kifupi.

Kwa mwaka huu utumiaji wa mfumo huo umekuwa ukiongezeka kwa wastani wa 700k kwa mwezi.

 “Wateja wetuj wanaweza kutumia program hiyo kufunguja mara moja akaunti ya Ecobank Xpress Account™, ambayo haihitaji malipo, hakuna matumizi ya karatasi, wala haja ya kuwa na kianzio au mabaki yenye kiwnago yanayohitajika na unaweza kupokea na kutuma fedha katika nchi 33 za Afrika,” alisema.

“Kwa hiyo, program yetu imeondoa vikwazo vyote ambavyo vimekuwa vikikwamisha mataifa mengi ya Afrika kufanya miamala ya kifedha na inatoa uwezo wa kutuma, kupokea na kufanya miamala mbalimbali kwa unafuu na urahisi.”  Aliongeza.

Mtendaji wa Ecobank anayeshughulikia huduma kwa wateja Patrick Akinwuntan, amesema benki yake imejikita katika kuhakikisha kwamba inawawezesha watu wote wa Afrika kuwa na huduma za fedha zenye ufanisi zilizoungwa na mawakala.

 “Tunataka kuwa benki chaguo la waafrika wengi kw aubora wa huduma za kibenki za kidigitali,” alisema.

“Utendaji ni kitu kingine na kuwapa wateja huduma muafaka isiyowasumbua ni  kitu kingine. Kuwapo kwa mawakala wa Ecobank jirani nawe kunakuwezesha kutumbukiza fedha katika akaunti yako ya Ecobank Xpress na kuanz akufanya malipo kwa  njia ya mtandao  ukitumia Ecobankpay. Pia unaweza kutoa fedha  kw akutumia fedha za nchi  husika hata kama zimeletwa kwako kutoka nchi nyingine kwa kutumia huduma yetu yenye ubunifu wa hali ya juu ya kuhamisha miamala.”

Huduma hii ya Ecobank Mobile App  inaweza kupakuliwa kutoka katika Google Play Store au Apple Store.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad