HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 3 April 2018

DAWASCO YAWAOMBA WALIOUNGANISHIWA MAJI MRADI WA WACHINA KUJISAJILI BURE

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
MENEJA wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam(DAWASCO)Ubungo Mhandisi Paschal Fumbuka amewaomba wakazi waliounganishiwa maji kupitia mradi wa Wachina kujisajili katika ofisi husika bure kabisa.

Akizungumza na Michuzi blog leo jijini Dar es Salaam Fumbuka ameeleza zaidi ya wateja 250 hawajasajiliwa ila wanatumia maji kupitia idara hiyo, ameeleza mradi huo wa Wachina ulilenga kutoa huduma ya maji kwa wakazi wote katika mfululizo wa vipindi vinne kuanzia mwaka 2011 na wa sasa wanahitaji takwimu ya watumiaji wa maji hayo katika maeneo mbalimbali
.
Aidha Fumbuka ameeleza kama DAWASCO wameandaa dawati maalumu la usajili wa wateja hao na baada ya hapo watalipa bili za kawaida kama wateja wengine.

Kuhusu  maafisa wa DAWASCO kuhusika katika hujuma ya  kuuza maji kwa baadhi ya maeneo baada ya kukata maji Fumbuka amekanusha suala hilo na kueleza kuwa jiografia hupendelea maeneo yenye mabonde hivyo maji yakikatika  hukimbilia sehemu zenye mabonde na hudumu kwa siku 2 au 3 na baadhi ya maeneo hupata maji hivyo hakuna hujuma katika hili.

Pia ameeleza kuwa wana mpango mkubwa wa kufikisha huduma ya maji kwa wakazi wote na kwa asilimia 61 wamefanikiwa na kwa sasa wapo katika hatua za mwisho za mradi wa maji katika maeneo ya Makabe, Msigani na Kwembe.
 Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka, akizungumza na Michuzi Blog leo jijini Dar es Salaam juu ya wakazi wa Dar es salaam waliounganishiwa maji kupitia mradi wa Wachina kujisajili katika ofisi husika bure.
 Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka akionesha vifaa mbalimbali.(Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii)
Meneja wa  (DAWASCO) Ubungo, Mhandisi  Paschal Fumbuka (kulia) akiwa na Meneja Juma Kalemera wakionesha mabomba ya ukubwa tofauti ambayo yapo tayari kwa matumizi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad