HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, April 27, 2018

CSI yatoa msaada wa vifaa tiba kwa wakina mama wajawazito hospitali ya Mnazi Mmoja

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
TAASISI ya Childbirth Survival International (CSI) imetoa wa vifaa vya akina mama wajawazito ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

Lengo la msaada huo ni muendelezo wa CSI wa kuendelea na jitihada zao za kufanikisha uzazi salama nchini huku moja ya jukumu lao kubwa ni kuhakikisha vifo kwa mama mjazito na mtoto mchanga vinapungua au kwisha kabisa.

Akizungumza leo baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mmoja wa Waanzilishi na Mkurugenzi Mkazi nchini Tanzania Stella Mpanda amesema wamekuwa na utaratibu wa kusaidia na kutoa vifaa vya kujifungulia katika hospitali mbalimbali na sasa wameona ni vema wakatoa msadaa huo Hospitali ya Mnazimmoja.

"Tumeamua kusaidia vifaa hivi kwani nia yetu ni kuona mama mjazito na mtoto mchanga wanakuwa salama.Vifaa ambavyo tumekabidhi leo vitarahisisha mkunga kuwa na uhakika wa vifaa na hatimaye mama mjazito kujifungua salama.

"Ni vifaa ambavyo vimetimia kwani ndani yake kuna kila kitu kikiwemo kifaa cha Peguine Pum ambayo husaidia kumsafisha mtoto mara tu baada ya kuzaliwa kwani huondoa uchafu ambao huenda ameuvuta.

"Ni vifaa vyenye gharama lakini CIS tunaahidi tutendelea kulera vifaa vya akina mama wajawazito kadri tunavyoweza.Tunataka mama mjazito kabla na baada ya kujifungua anakuwa salama na hilo ndilo jukumu letu,"amefafanua Mpanda.

Amefafanua kuwa wanatambua jitihada ambazo Serikali inafanya katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga lakini nao CSI wamekuwa na jukumu hilo kwa muda mrefu katika kujikita wanatoa elimu ya uzazi salama ili kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

Kwa upande wa Hospitali ya Mnazi mmoja umesema vifaa hivyo vimekuja wakati muafaka na vitasaidia katika kutoa huduma za uzazi hospitalini hapo.

Wameipongeza CSI kwa kutambua na kuipa umuhimu hospitali hiyo ambayo wameilezea imekuwa ikipokea wajawazito wengi kwa siku ambao wanakwenda kwa ajili ya kujifungua.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akikabidhi msaada wa vifaa vya akina mama wajawazito kwa Dk. Fillo Hyera (wa tatu kushoto) ambavyo hutumika wakati wa kujifunga katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI), Stella Mpanda(wa kwanza kulia) akimkabidhi Mama Mjamzito. Yusta Prospa moja ya kifaa tiba ambacho hutumika wakati wa kujifungulia katika Hospitali ya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam leo.
 Dk. Fillo Hyera(kulia) akitoa shukrani kwa  uongozi wa Taasisi ya Childbirth Survival International (CSI) mara baada ya kukabidhi vifaa tiba vya wakina mama wajawazito.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad