HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 10, 2018

CHANETA YAANZISHA PROGRAMU YA KUHAMASISHA MCHEZO WA NETBALI NCHI NZIMA

Na. Jumbe Ismailly 
CHAMA cha Netbal Tanzania (CHANETA)  kimeanzisha Program maalumu ya kuhamasisha mchezo wa Netball kuanzia ngazi ya wilaya, Mkoa hadi Taifa  ili kuhakikisha kiwango cha mchezo huo kinakua kwenye maeneo yote nchini badala ya sasa ambapo baadhi ya mikoa mchezo huo umeanza kutoweka kabisa.
Mjumbe wa Chaneta Taifa, Yasinta Silivester aliyasema hayo kwenye mafunzo ya walimu wa mchezo wa Netball yaliyohudhuriwa na walimu 19 wa shule za msingi na sekondari wa Mkoa wa Singida na kufanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenge mjini Singida.

“Mheshimiwa mgeni rasmi chama cha netball kimekuwa na Program sasa hivi ya kuhamasisha mchezo wa netball kuanzia ngazi ya wilaya,Mkoa hadi Taifa”alisisitiza Yasinta.

Kwa mujibu wa Yasinta mwezi wa nane,mwaka huu kutakuwa na semina ngazi ya taifa,hivyo walimu waliohudhuria mafunzo hayo yaliyofanyika shule ya sekondari Mwenge,angependa wasinyimwe ruhusa ya kuhudhuria mafunzo hayo yatakayofanyika Mkoani Manyara.
Hata hivyo kiongozi huyo wa kitaifa alisisitiza kwamba ni muhimu kwa walimu hao wakahudhuria kwenye mafunzo hayo ya kitaifa kutokana na Mkoa wa Singida kuwa bado upo nyuma sana katika mchezo wa netbali.

“Meshimiwa mgeni rasmi mimi kama mjumbe wa taifa wa chaneta nasimamia kanda za Kaskazini na kanda ya kati  yenye mikoa ya Manyara,Singida,Arusha,Kilimanjaro na Dodoma,kwa hiyo mwezi huu kulikuwa na semina ngazi ya basic ya Mkoa Kilimanjaro ,Manyara walifanya mwaka jana na mwaka huu Singida mwezi wa nane kutakuwa na semina ngazi ya taifa”aliweka bayana mjumbe huyo wa chaneta taifa.

Akizungumza na walimu wa michezo waliohudhuria mafunzo hayo ya siku tano,Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Martin Kapera pamoja na mambo mengine alitumia fursa kuvipongeza vituo  vya Televisheni vya Channel Ten Azamu kwa mchango wake wa kutangaza michezo katika Mkoa huo.
 Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo.Grace Irumba alisisitiza kwamba mchezo huo wa Netbali kidogo ulikuwa kama vile unataka kulala lala,lakini kwa uwezo wake Mungu uongozi wa Taifa na viongozi uliopo mikoani kila mmoja anataka kuuamsha mchezo huo katika Mkoa wake.

Katika risala ya wanasemina hao iliyosomwa na Luiza Mujah iliyataja malengo ya mafunzo hayo kuwa ni pamoja na kupata ujuzi wa uamuzi wa mpira wa Netbali unaoendena na sheria mpya za mpira wa Netbali ili waweze kuutumia ujuzi huo kwenye maeneo yao                                                   
 Mjumbe wa kamati ya utendaji Taifa CHANETA,Yasinta Silivester akizungumza na walimu 19 waliohudhuria mafunzo ya siku tano ya mchezo wa Netiball yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa shule ya sekondari Mwenye, mjini Singida.
 Afisa michezo wa Mkoa wa Singida,Henry Kapera akisaini vyeti vya kuhitimu mafunzo kwa walimu wa michezo wa Netibali Mkoani Singida.
 Mwalimu Luiza Mujah (mwenye fulana ya njano) akikabidhiwa na Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera cheti cha kuhitimu mafunzo ya mchezo wa Netibali.
Washiriki wa mafunzo ya mchezo wa Netibali wakiwa kwenye picha ya pamoja na Mgeni rasmi,ambaye pia ni Afisa Michezo wa Mkoa wa Singida, Henry Kapera(aliyevaa fulana nyekundu), viongozi wa Chaneta Mkoa na Taifa. (Picha zote Na Jumbe Ismailly)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad