HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 10 April 2018

"BQ CONTRACTOR" YANYAKUA TUZO YA UBORA YA KIMATAIFA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura (wa pili kutoka Kulia) akiwa amenyanyua Tuzo ya Ubora ya Kimataifa (ISO 9001:2015) Baada ya Kampuni yake kukidhi viwango vya Kimataifa, baada ya kukabidhiwa na Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa  (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi (kushoto), katika hafla fupi iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere, jijini Dar es salaam leo. Mengine pichani ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa Contractors Association of Tanzania, Injinia Lawrence Mwakyambiki.
Mwenyekiti wa Contractors Association of Tanzania, Injinia Lawrence Mwakyambiki (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura, Tuzo ya Ubora ya Kimataifa (ISO 9001:2015) kwa niaba ya Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi (kushoto). Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori
Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi akiwasilisha mada katika mkutano wa Wakandarasi, uliofanyika
kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Julias Nyerere, jijini Dar es salaam leo
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura wa pili kutoka Kulia akieleza manufaa ya Tuzo hiyo ya Ubora wa Kimataifa baada ya Kukabidhiwa. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), Rhoben Nkori Kushoto ni Meneja wa Biashara wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Hilu Bura na Katikati ni Mtaalam wa Mawasiliano na Msaidizi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya BQ Injinia Lorenco Simon.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura (wa pili kutoka Kulia) akikabidhi Tuzo ya Ubora ya Kimataifa (ISO 9001:2015) waliyoshinda, kwa mmoja wa wafanyakazi kwa kampuni hiyo.
Mkaguzi wa Ubora wa Mifumo ya Kimataifa (AQC Midle East FZE), Alfred Lihasi (kushoto) akizungumza jambo wakati akiielezea Tuzo Hiyo ya Kimataifa kabla ya Kuikabidhi kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Ukandarasi ya BQ, Injinia John Bura (wa Pili Kushoto).
Wakurugenzi wa Makampuni Mbalimbali wakiwa katika picha ya Pamoja baada ya Kampuni ya Ukandarasi ya BQ kukabidhiwa Tuzo ya Ubora wa Kimataifa jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad