HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 20 March 2018

WAZIRI WA MAJI AZUNGUMZIA UMUHIMU WA KUKABILIANA NA UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI, MAZINGIRA

Na Leandra Gabriel, Globu ya jamii
WAZIRI wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema ni muhimu kuwekwa mikakati ya kukabiliana na uharibifu unaoendelea katika vyanzo mbalimbali vya maji na misitu nchini.

Mhandisi Kamwele amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Maji Duniani na kwa Tanzania lengo lake ni kuangalia uwezekano wa kuwapatia maji safi na salama kwa watanzania wote.

Aidha ameeleza mkakati wa kuvuna maji ya mvua ili kupata maji shuleni kupitia matanki na visima vya kujenga ambapo anaamini itasaidia kuondoa changamoto ya uhaba wa maji shuleni.

Pia ameeleza mafanikio katika suala la maji na majengo katika shule za Kirumba na Isenyi jijini Mwanza pia katika ujenzi wa vyoo na vyumba kwa wanafunzi wa kike.

Ameshukuru Benki ya dunia, Serikali ya Korea  na Mpango wa maendeleo Ufaransa kwa ushirikiano wao katika suala la maji na utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji ni lazima.

Amesisitiza Serikali ya Awamu ya tano imedhamiria kuleta mapinduzi katika kutokomeza umaskini ikiwemo katika kutatua suala la upatikanaji wa maji.

 Pia amehimiza ushirikiano baina ya wanajamii katika suala la ukataji miti na uharibifu wa misitu.

Naye Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini Profesa Uswege Minga amesisitiza utunzaji wa maji kwani matumizi yake ni makubwa zaidi ya kupika na kunywa na amesisitiza utunzaji wa maji na vyanzo vyake sambamba na matumizi sahihi ya maji.

Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wadau wa maji uliandaliwa na benki ya Dunia nchini uliokwenda kwa jina la 'TANZANIA WASH POVERTY DIAGNOSTIC' uliofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
 Mkurugenzi mkazi wa Benki ya Dunia Tanzania, Malawi na Burundi, Bella Bird akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji kufungua mkutano huo muhimu kwa ajili ya maji Tanzania.
 Mwasilishaji wa mada juu ya kupinga umaskini na uhaba wa maji  Mchumi wa Benki ya Dunia, George Joseph akizungumza na wadau wa maji waliofika katika mkutano huo.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tumaini(TUDARCO), Prof.  Uswege  Minga  akizungumzia na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa utunzaji wa maji na na mazingira kwa ajili ya kizazi cha sasa na baadae.

Baadhi ya Wadau wa Maji wakifatilia kwa ukaribu Mkutano wa Benki ya Dunia wa masuala ya maji uliofanyika jijini Dar es Salaam leo kama sehemu ya maadhimisho ya wiki ya maji.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad