HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 14 March 2018

WATU NANE WANASHIKILIWA NA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI NYAMAGANA.

KWAMBA TAREHE 13.03.2018 MAJIRA YA SAA 16:30HRS JIONI KATIKA MTAA WA MABATINI KUSINI KATA YA MABATINI WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU NANE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.DEUS LUCAS, MIAKA 52, DIWANI WA KATA YA MABATINI - CHADEMA, 2. DANIEL MONGO, MIAKA 46, MWENYEKITI CHADEMA TAWI LA KILOLELI B”, 3. LAURENCE CHILO, MIAKA 21, MFANYABIASHARA NA MKAZI WA MTAA WA MABATINI, 4.LAMECK KAUNDA, MIAKA 38, MKAZI WA KILOLELI B, 5.JACKSON MADEBE, MIAKA 44, MKAZI WA MTAA WA MWANANCHI, 6.BI SECILIA BUTUKO, MIAKA 4O, MKAZI WA MTAA BUGARIKA, 7.MWITA SAGALI, MIAKA 38, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA NA 8.SELEMAN GABRIEL, MIAKA 45, MKAZI WA MTAA WA BUGARIKA, WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUFANYA MKUSANYIKO WA KISIASA BILA KIBALI, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.

AWALI POLISI WALIPOKEA TAARIFA TOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA MTAA TAJWA HAPO JUU LIPO KUNDI LA WATU KATI YA 200 NA 500, WAFUASI WA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) WAMEKUSANYIKA KATIKA NYUMBA ALIPOPANGA BWANA LAURENCE CHILO, HUKU WAKIWA WAMEFUNGA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO (CHADEMA) NA SPIKA ZA MATANGAZO. HUKU WANACHAMA  HAO WA CHADEMA WAKIDAI KUWA WAMEKWENDA KUMUHANI MWANACHAMA MWENZAO BWANA LAURENCE CHILO ALIYEPATWA NA MSIBA WA KUFIWA NA MAMA YAKE MZAZI MIEZI SITA ILIYOPITA KATIKA HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE KISHA KWENDA KUZIKA NYUMBANI KWAO UTEGI WILAYANI TARIME MKOANI MARA MWAKA JANA.

AIDHA BADAE ILIDAIWA KUWA JAMBO LILILOKUWA LIKIENDELEA KATIKA KIKAO HICHO NI UGAWAJI WA KADI ZA CHAMA, KUANDIKISHA WANACHAMA WAPYA NA KUTOA HOTUBA. ASKARI WALIFIKA KATIKA ENEO LA TUKIO KISHA KUWAITA VIONGOZI NA  KUONGEA NAO ILI KUWEZA KUFAHAMU UHALALI WA KIKAO HICHO NDIPO GHAFLA WALIANZA KURUSHA MAWE KWA ASKARI. ASKARI WALIWEZA KUJIHAMI VIZURI KISHA WALIFYATUA MABOMU YA MACHOZI HEWANI KUWATAWANYA NA BAADAE WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WAFUASI NANE TAJWA HAPO JUU  WA CHAMA HICHO.

KATIKA ENEO LA TUKIO KUMEPATIKANA BENDERA ZA CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO, KADI ZA CHADEMA ZILIZOANDIKWA MAJINA NUSU, KADI ZA CHADEMA AMBAZO HAZIJAANDIKWA MAJINA NA KADI ZILIZOANDIKWA MAJINA, MIHURI MIWILI, KARATASI TATU ZENYE MAJINA YA MAHUDHURIO NA T-SHIRT ZENYE NEMBO YA CHADEMA. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WAWILI PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMNI. UFATILIAJI WA KUHAKIKISHA MJI UNAKUWA SHWARI UNAENDELEA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA VIONGOZI WA SIASA NA WANACHAMA WAO KWA UJUMLA AKIWATAKA KUACHA TABIA  ZA HOVYO AMBAZO ZIPO KINYUME NA SHERIA NA TARATIBU ZA NCHI ZENYE LENGO LA KUONDOA UTULIVU KATIKA MKOA WETU.

 KWANI SUALA HILO HALIKUBALIKI NA TUTAWASHUGHULIKIA WOTE WANAOKWENDA KINYUME NA SHERIA ZA NCHI. PIA EMEOMBA WANANCHI WAELEWE KUWA AMANI NA UTULIVU NA USALAMA MKOANI KWENTU NA NCHI YETU KWA UJUMLA NI JAMBO LA MSINGI.

 BILA UTULIVU, AMANI NA USALAMA HAKUTAKUWEPO NA SHUGHULI YEYOTE YA MAENDELEO ITAKAYOFANYIKA KWA HIYO TUEPUKE WALE WOTE WANAOSHAWISHI VURUGU/FUJO. PIA ANAWAOMBA WANANCHI WAENDELEE KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU WA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad