HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, March 25, 2018

WANANCHI DODOMA WAAMKA VITAMBULISHO VYA TAIFA

Wananchi mkoani Dodoma wameendelea kufurika kwenye vituo vya Usajili mkoani humo kushiriki zoezi la Usajili wa Vitambulisho vya Taifa linaloendeshwa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa- NIDA.

Zoezi hilo ambalo limelenga kuwasajili wananchi wote wenye umri wa miaka 18 na kuendelea limeonekana kuwavuta wananchi kwa wingi tofauti na ilivyokuwa siku za nyuma wakitokea maeneo mbalimbali ya mkoa huo na viunga vyake.

Kata ya Chamwino na Chang’ombe zilizopo Wilaya ya Dodoma mjini leo zimetia fora kwa maelfu ya wananchi waliomiminika alfajiri kupata huduma hiyo huku baadhi wakionekana kwenye mitaa ya mji huo wakihaha kutoa nakala (copy) ya viambatisho vyao kwenda kujaza fomu.
Akizungumzia mwenendo wa zeozi hili ambalo lilianza tangu mwezi Februari,2018; Mtendaji wa Kata ya Chang’ombe Bi. Neema Makinda amesema mwitikio wa watu ni mkubwa na wamejipanga kuwahudumia wananchi wote wa Kata hiyo ambao idadi yao ni Zaidi ya elfu 25.

“ hapa bado; unavyowaona hapa hawajafika hata robo, tunaendelea kuwahamasisha ili kuhakikisha hakuna mwananchi hata mmoja atakayeachwa kwenye zoezi hili kwani umuhimu wake tunaufahamu” alisisitiza

Mkoa wa Dodoma ni miongoni mwa mikoa 20 ya Tanzania inayoendelea na zoezi la kuwasajili wananchi na wageni wanaoishi kihalali nchini na kuwapatia Vitambulisho vya Taifa; zoezi ambalo kwa Dodoma linatazamiwa kumalizika mwanzoni mwa mwezi Mei mwaka huu.
 Mtendaji  wa Kata ya Chang’ombe Bi. Neema Makinda akimpitishia fomu mmoja wa wananchi wa Kata hiyo aliyefika kwenye kituo cha Usajili kusajiliwa.
 Bw. Jumanne Bakari akikaguliwa fomu yake na Mwenyekiti wa Mtaa wake Bi. Havijawa Ramadhani ( wa kwanza kushoto) na pembeni yake ni Bi. Tatu Kimwaga mjumbe wa Mtaa.
 Baadhi ya wananchi wa Kata ya Chamwino wakiwa wamejipanga kwenye foleni  kwenye viwanja vya wazi nje ya Shule ya Msingi Chamwino wakisubiri kusajiliwa  Vitambulisho vya Taifa.
 Bi. Asha Twaha Mruma, mwananchi katika Mtaa wa Chamwino akiwa anajaza fomu ya maombi ya Vitambulisho vya Taifa huku pembeni mtoto wake mdogo wa kiume akishuhudia mama yake akijaza fomu hiyo kwa umakini mkubwa.
Wananchi wa Kata ya Chamwino wakiwa wamejipanga foleni fotauti tofauti kupata huduma. Baadhi wakiwa kwenye foleni ya kujaza fomu na kugonga mhuri wa Mtendaji wa Mtaa na Kata na wengine wakielekea mahali mashine ziliko kwa ajili ya kupigwa picha, kuchukuliwa alama za vidole na saini ya kielektroniki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad