HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 20, 2018

WAKAZI WA KATA TANO DAR WAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUINGILIA KATI UBOMOAJI WA NYUMBA ZAO

Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
WAKAZI wa Kata  tano  wa Jiji la Dar es Salaam wamemuomba Rais Dk. John Magufuli kuingilia kati ubomoaji wa  nyumba kata hizo katika kupisha ujenzi wa bomba la Maji la Ruvu.

Kata zitazoathirika kwa makazi katika upanuzi wa ujenzi wa bomba la Ruvu Juu ni Wazo, Salasala, Bunju Mbweni pamoja na Mabwepande

Akizungumza na waandishi wa habari mkazi wa Salasala Dk. Julian Bujugo amesema hawapati usingizi tangu walivyoambiwa wavunje nyumba zao wakati sheria inawalinda.

Amesema sheria ya mwaka 2001 ya Dawasa katika ujenzi wa mabomba yao ni mita tano (5) lakini sasa wameambiwa ni mita 15 ambazo hiziko katika sheria 

Bujugo amesema kuwa katika suala hilo walitaka kwenda mahakamani lakini waliona wazungumze ili kuweza kusema kwa Serikali kitu ambacho kinawatatanisha kuhusu  uboaji huo.

Amesema kuwa Rais Dk.Magufuli ni mtetezi wa wanyonge,hivyo kwa wakazi wa kata tano jicho lao ni kwa Rais na  sheria inawafanya kuwa halali.

Bujugo amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kuangalia suala lao kwani hawana sehemu ya kukimbilia.
Mkazi wa Salasala na Diwani wa Kata ya Magomeni, Dk.Julian Bujugo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na ubomoaji wa nyumba zao ambapo ni kinyume cha sheria  jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad