HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 27, 2018

WAHAMIAJI HARAMU WAKAMATWA PINGO/MKOANI PWANI-RPC SHANNA


Wahamiaji haramu kutoka nchini Ethiopia ambao wamekamatwa na jeshi la polisi Mkoani Pwani ,huko porini Pingo shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze.
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akizungumza kuhusiana na misako na doria zinazoendelea Mkoani humo.
 Kamanda wa polisi Mkoani Pwani, (ACP) Jonathan Shanna akiakionesha baadhi ya siraha alizokamata.

Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
JESHI la polisi mkoani Pwani, limewakamata wahamiaji haramu kumi raia wa nchi ya  Ethiopia ,kwa kosa la kuingia nchini bila kibali.

Jeshi hilo pia, limemtia nguvuni mwanamke -Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye silaha aina ya shortgun, huko kijiji cha Manda Mazingara kata ya Miono,tarafa ya Mkange wilaya ya Bagamoyo.

Kamanda wa polisi mkoani Pwani, (ACP), Jonathan Shanna alisema, wahamiaji haramu hao wamekamatwa machi 26, wakiwa porini ,Pingo Shule ,wilaya ya kipolisi Chalinze na askari waliokuwa doria kufuatia kupata taarifa kutoka kwa raia wema.

Akielezea matukio mbalimbali yaliyotokea mkoani hapo, aliwataja waliokamatwa kuwa ni Tagen Alam (19), Abraham Wolde (19) na Musama Kamal (16).

Wengine ni Abush Tamaskel (16), Ayela Erapo (18) na Ngusie Kechine (18), Zarabel Faisa (16), Tsedhj Yshgee (19), Teyey Ally (18) na Tuktigo Clemag (17).

Watuhumiwa wote hao watafikishwa idara ya uhamiaji kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Kamanda Shanna alielezea ,jeshi hilo linaendelea na juhudi za kuwatafuta watu waliowasaidia kuingia nchini bila kufuata utaratibu wa sheria.

Katika tukio jingine , mwanamke aliyejulikana kwa jina la Felister Mtinga (30-36) amekutwa kitandani akiwa amefariki dunia katika nyumba ya kulala wageni iitwayo Moreto,iliyopo Chalinze.

Kamanda Shanna alisema kuwa, mwili wa mwanamke huyo ulibainika machi 26 mwaka huu majira ya saa nne asubuhi baada ya wahudumu kutomuona akitoka tangu alipoingia ndani machi 25 katika nyumba hiyo.

Alifafanua , mwili wa marehemu umeshafanyiwa uchunguzi wa awali na kubaini kutokuwa na majeraha ya aina yoyote hali inayosababisha kuondoa mashaka kuhusu kifo chake na umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Tumbi.

Katika tukio la kukutwa na silaha, kamanda Shanna alibainisha wamekamata silaha mbalimbali katika misako inayoendelea kufanyika mkoani hapo, ikiwemo SMG .R.6134, mapanga manne, sime moja na risasi 23.

Alieleza, saa sita usiku machi 27,walimkamata mwamke aliyetambulika kwa jina la Siwema Mgombale akiwa na risasi 23 zinazotumika kwenye short gun na Ramadhani Mdoe akiwa na silaha aina ya SMG.R.6134 .

“Tunaendelea na misako kabambe inayoongozwa na kikosi chao cha siri, tunafanya misako uvungu kwa uvungu,giza kwa giza,pori kwa pori,tunashukuru inazidi kufanikiwa na ni endelevu “alisisitiza kamanda huyo.

Kamanda Shanna aliwaomba wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kutoa taarifa za wale wachache ambao wanawadhania ni wahalifu kwenye maeneo yao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad