HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, March 5, 2018

UMOJA WA MATAIFA YAIMWAGIA SIFA JWTZ NA SERIKALI YA JPM


Na Luteni Selemani Semunyu,  UNAMID
Umoja wa mataifa UN umeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais John Magufuli na Mkuu wake wa Majeshi  ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kufuatia jitihada zao za kudumisha amani ndani na Nje ya Nchi hiyo.

Hayo yalibainishwa na mwakilishi Malum wa katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia masuala ya Watoto (Special Representative of Secretary general of Child Abuse and AA) Profesa Virginia Gamba wakati wa Ziara yake kikazi katika Maeneo ya vjiji vya Shangilitobaya Jimboni Darfur nchini Sudan hivi Karibuni.

Alisema Tanzania ni miongoni mwa nchi ya kuigwa Afrika zinazopiga hatua kubwa ya maendeleo zinazopaswa kutiliwa mfano lakini  yote hiyo inatokana na umadhubuti wa Serikali yake, na Jeshi la ulinzi la Wananchi wa Tanzania kwa mchango wake  katika kushughulikia mambo ya msingi katika kudumisha Amani.

“Sina budi kuipongeza Serikali chini ya rais John Magufuli inafanya kazi nzuri na Mkuu wa majeshi ya Ulinzi Jenerali Venance Mabeyo kwani utendaji wao ni wa kutukuka Afrika nzima katika kuleta Amani kwani bila Amani hakuna maendeleo hivyo maendeleo yanayotarjiwa Tanzania ytapatikana kwa sababu ya Amani” Alisema Profesa Virginia.

Aliongeza kuwa kutokana na kuimarika kwa Amani ni rahisi kwa nchi yeyote kujiletea maendeleo haraka na kuwataka kuendeleza jitihada hizo kwa kuwalinda watoto ambao ni nusu ya Idadi ya watu Duniani hivyo wakilindwa Watoto Dunia itakuwa salama.

“ Najivunia Tanzania naweza kujiita mi ni rafiki wa Tanzania sio kwa sababu nyingine ni kutokana na Umahiri wao katika Amani ikiwemo jeshi lake la Ulinzi limekuwa Msaada mkubwa katika kuleta Amani kupitia Umoja wa Mataifa” Alisema Profesa Virginia.

Pia aliwataka Wananchi wa Sudan kuiga Mfano wa Tanzania waliowasha mwenge katika kilele cha Mlima Kilimanjaro kuwa ishara ya Amani Afrika na kumulika dhidi ya maovu mbali mbali  ikiwemo dhidi ya watoto kwa kuwasha moto wa amani utakaoangazia watoto wote wa Sudan.

Aliongeza kuwa  ni wajibu wa Sudan kuuiga Tanzania kwa kuwasha moto wa Amani kwani wana kila sababu ya kufanya hivyo bila kutegemea msaada wowote kwani ni nchi yenye rasilimali nyingi za kiuchumi lakini kinachokwamisha ni Amani ili kujiletea maendeleo.

Mwakilishi huyo wa Umoja wa mataifa mbali na kutembelea vijiji mbalimbali alitembelea kambi ya Shangilitobaya inayokaliwa na Kikosi cha Tanzania chini ya kikosi cha 11 kinachoongozwa na Kanali William Sandy na kuwapongeza Askari wake kwa kazi nzuri ya Ulinzi wa Amani Duniani kote.

Tanzania kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linashiriki katika mpango wa Ulinzi wa Amani chini ya Mwamvuli wa Umoja wa mataifa na Umoja wa Afika UNAMID nchini SUDAN ambayo sasa inaingia hatua ya Pili ambayo majeshi ya Tanzania yameunganihswa katika kikosi maalum ambacho kinaanza kazi katika safu za Milima ya jebel Marra Mashariki maeneo ambayo hayakunufaika kwa kufikiwa na UNAMID kwa kipindi chote.

Wanajeshi wa Tanzania hivi karibuni walipongezwa kuyafikia maeneo ya  safu za Milima ya Jaber Mara na  kufanya Doria ikiwa ni kwa mara ya kwanza  kwa UNAMID na mashirika ya Umoja wa Mataifa kutokana na maeneo hayo kukaliwa na Waaasi na ubovu wa Miundombinu.
 Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID  wakiwa katika Doria maeneo ya Jirani na Mlima Mawe Khor Abeche Jimboni   Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).
 Mwakilishi maalumu wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia watoto na Migogoro ya Kivita Virginia Gamba akizungumza na Meja Afred Mwinuka wakati alipotembelea kambi ya  Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID  Shangilitobaya Jimboni   Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

Msafara Wanajeshi kutoka jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania wanaoshiriki Ulinzi wa Amani chini ya Mpango wa umoja wa mataifa na Umoja wa Afrika UNAMID  wakiwa katika Doria maeneo ya kijiji cha Shardai Jimboni  Darfur Nchini Sudan ( Picha na Luteni Selemani Semunyu).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad