HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 23, 2018

TBA YATAKIWA KUKAMILISHA UJENZI WA OFISI ZA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KWA WAKATI

Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Tume Jaji wa Rufaa, Mhe. Semistocles Kaijage wametembelea eneo la Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika eneo la Njedengwa mkoani Dodoma.

Mara baada ya kuwasili katika eneo la Mradi na kukagua maendeleo ya ujenzi wa jengo hilo wajumbe hao wameonyesha kutoridhishwa na kasi ya ujenzi ya Wakala wa Majengo nchini Tanzania (TBA) wanaojenga jengo hilo na kuwataka waukamilishe mradi huo kwa wakati kama ilivyopangwa.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad