HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, 26 March 2018

TAIFA STARS, CONGO KUKIPIGA KESHO UWANJA WA TAIFA

Na Agness Francis Blogu ya Jamii
BAADA ya Taifa Stars kuchapwa mabao 4-1 dhidi ya Algeri wakiwa ugenini sasa wanawakaribisha nyumbani kikosi cha timu ya Taifa ya Jamuhuri  kidemokrasia ya Congo kwenye mchezo wao wa kirafiki.

Mchezo huo wa aina yake kati ya timu hizo mbili utachezwa kesho Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 10 jioni na kiingilio kwa VIP ni Sh.5000 na viti vya mzunguko na vyenye rangi ya Chungwa ni Sh.1000.

Akizungumza leo Dar es Salaam, Kocha Msaidizi wa timu ya Taifa Stars  Hemedi Moroccoleo, amesema mchezo utagumu kwao lakini amewahakikishia Watanzania kupata ushindi katika mchezo huo.

"Tunatarajia kufanya vizuri katika mchezo wa kesho ili kupata ushidi ili kusogea mbele kuwa kwenye nafasi nzuri  tutajitahidu kadri ya uwezo wetu kupambana kwa kuwa wenzetu wacongo wako vizuri na makini katika mchezo wa Soka" amesema kocha Morocco.

Kocha Morocco amesema katika mtanange huo wa kesho kikosi chake kipo fiti kumenyana na Timu ya taifa ya Congo,isipokuwa mchezaji mmoja tu Abdulaziz Makame ambaye ni majeruhi ana maumivu ya henka ataukosa mchezo huo.

Mchezaji wa kikosi cha Taifa stars Himidi Mau amesema kuwa kwa niaba ya wachezaji wenzake wako tayari  kupambana na mechi ya kesho dhidi ya kikosi hicho ili kuhakikisha wanafanya vizuri na  wanapata ushindi wakiwa nyumbani.

Kwa upande wa Kocha Ibenge Florent wa Timu ya Taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasiya ya Congo amesema mchezo wa kesho utakuwa mgumu na wa aina yake ila anakiamini kikosi chake kipo vizuri kwa ajili ya kupambana na Taifa Stars katika mchezo huo wa kirafiki.

Meneja masoko wa Serengeti Brewer Nicolaus Machugu amewataka watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuishangilia Taifa Stars.
 Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemedi Morocco akizungumza na waandishi wa habari Leo katika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) kuhusu maandalizi ya kumenyana na Timu ya Taifa ya Jamuhuri ya Kidemokrasiya ya Congo katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa kesho uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.
 Kocha Mkuu wa Timu ya Congo, IBenge Florent akizungumza na wandishi wa habari leo katika makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa miguu  Tanzania (TFF) akizungumzia ujio wao pamoja na maandalizi katika mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Timu hizo mbili utaokachezwa katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Da ea Salaam.
Mchezaji wa Taifa Stars, Himidi Mau akizungumza na wandishi wa habari kwa ni aba ya wenzake   kuelekea kesho kwenye dimba la uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam  katika  mchezo wa kirafiki na Kikosi cha Congo Leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF).
Nahodha wa Kikosi cha Timu ya Congo, Benic Adobe akizungumza na wandishi wa habari leo makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusu maandalizi ya mechi hiyo itakayochezwa kesho katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a comment

Post Bottom Ad