HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 3, 2018

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA KALI WAKANDARASI WOTE WALIOHUJUMU MIRADI YA MAJI

Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ameitaka Bodi ya Usajili ya Wakandarasi nchini (CRB) kuwachukulia hatua kali wakandarasi wote walioihujumu Serikali katika miradi ya maji inayotekelezwa nchini.
Naibu Waziri Aweso ametoa tamko hilo mara baada ya kufanya kikao na bodi hiyo na kutaka ufanyike uchunguzi wa kwa miradi yote ambayo utekelezaji wake umegibikwa na utata na wakandarasi wote watakaobainika kutekeleza miradi hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.
Amesema hatuwezi kufika popote tukiendelea kuwalea wakandarasi wasio na uwezo ambao wamekuwa kikwazo katika utekelezaji wa miradi ya maji, hatutawaendekeza tena wakandarasi wa aina hii, kwa kuwa wamekuwa chanzo cha kukwamisha juhudi za Serikali katika kuiletea nchi maendelo.
‘‘Naomba mfanye uchunguzi wa kina katika miradi yote ya maji iliyohujumiwa nchini, wizara yangu itawapa ushirikiano wa kutosha ili tuweze kuwabaini wakandarasi waliohusika na ikithibitika kuwa ni kweli wachukuliwe hatua kali na ikibidi wafutiwe usajili kabisa’’, alisema Aweso.
Hata hivyo, amesema wako pamoja na wakandarasi wazawa na watarajie ushirikiano wa dhati kutoka kwa Serikali. Tutawapa kipaumbele wakandarasi wazalendo kwenye miradi ya Serikali na walio waaminifu tutawapa kazi zaidi, tutasimamia na kuhakikisha fedha zao zinalipwa kwa wakati ili watimize majikumu yao kwa ufanisi.
Naye, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi nchi, Joseph Tango amesema watafanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali wakandarasi wote waliohujumu miradi ya maji na watawasimamia wakandarasi wanaotekeleza miradi yote nchini kwa mujibu wa sheria na kanuni bila upendeleo kwa mkandarasi yeyote.
Aidha, Naibu Waziri wa Maji na UMwagiliaji ametembelea ofisi za Bohari Kuu ya Maji zilizopo Boko, jijini Dar es Salaam kwa dhumuni la kujionea shughuli zake pamoja na kuongea na watumishi wake kwa nia ya kujua mafanikio na changamoto zao.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akizungumza katika kikao cha pamoja na Wakurugenzi wa Bodi ya Usajili ya Wakandarasi (CRB) katika ofisi za bodi hiyo, kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CRB, Joseph Tango na wajumbe wengine wa CRB.
 Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiangalia bomba la maji lililopo kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji, nyuma yake ni Boharia Mkuu, Crepin Bulamu.
Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso akiwa kwenye karakana ya Bohari Kuu ya Maji iliyopo Boko, jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad