RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Fatma Gharib Bilal ambaye ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto.
Mwengine aliyeapishwa ni Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais.
Hafla hiyo, ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali akiwemo Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said pamoja na Mawaziri.
Viongozi wengine waliohudhuria hafla hiyo ni Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih, Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.
Katika maelezo yao viongozi hao mara baada ya kuapishwa waliahidi kutekeleza majukumu yao kwa mashirikiano ya pamoja kati yao na viongozi wengine wote wa Serikali wakiwemo wale wa Wizara zao pamoja na Ofisi watakazoziongoza.

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Fatma Gharib Bilal kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya
Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto katika hafla iliyofanyika leo
ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
akimuapisha Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa
Ikulu Mjini Zanzibar
Baadhi
ya Mawaziri waliohudhuria katika hafla ya kuapishwa Viongozi leo katika
ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein aliwaapisha Viongozi hao Fatma
Gharib Bilal kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya
Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi
kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(kushoto) akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais Mhe.Balozi Seif Ali
Iddi kabla kuwaapisha Viongozi aliowateuwa hivi karibuni hafla hiyo ya
kiapo ilifanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.
Miongoni
mwa Viongozi waliohudhuria katika kiapo cha Viongozi Fatma Gharib
Bilal kuwa Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Wanawake
na Watoto na Nd,Abdalla Hassan Mitawi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,walioapishwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)
katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo. (Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment