HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 13 March 2018

MTI WA MBUYU ULIOSHI KWA ZAIDI YA MIAKA 100 WAANGUKA MAENEO YA OCEAN ROAD JIJINI DAR


 Baadhi ya wananchi wakiangalia Mbuyu ulioanguka kufunga mawasiliano ya barabara inayotumiwa na viongozi wa wakuu wa serikalini ulioanguka leo jijini Dar es Salaam.
 Mti wa Mbuyu wenye miaka zaidi ya 100 ukiwa umeanguka na kufunga barababra ya Chimala na kusababisha kukatika kwa mawasiliano ya barabara pamoja na nishati ya Umeme leo  karibu na Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.

Mafundi wa Umeme wa Tanesco wakiwa katika eneo ulioanguka Mbuyu ambao ulifanya hitilafu ya nyaya za umeme leo jijini Dar es Salaam.
(Picha na Emmanuel Massaka)Na Chalila Kibuda,Globu ya jamii
KISHINDO kikubwa kimesikika katika maeneo ya barabara ya Chimala karibu na Hospitali ya Ocean Road baada ya mti wa mbuyu uliopo ndani ya uzio wa hospitali hiyo unaodaiwa kuishi zaidi ya miaka 100 kuanguka jijini Dar es Salaam.

Mbuyu huo umeanguka leo majira ya saa kumi alasiri ambapo baada ya kuanguka ulisababisha kukatika kwa nishati ya umeme katika maeneo hayo ya hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.Kuanguka kwa Mbuyu huo umesababisha pia sehemu ya uzio wa hospitali hiyo kuvunjika.

Hata hivyo licha kuanguka na kufunga barabara ambayo imekuwa mara nyingi ikitumika kupitisha magari ya viongozi wa ngazi mbalimbali Serikali, wakati huo hakukua na gari ya aina yoyote iliyopita.Hivyo hakukuwa na madhara zaidi ya kubomolewa kwa uzio wa Hispitali ya Ocean Road.

Baadhi ya mashuhuda wakati mbuyu huo unaanguka wamedai kabla ya kuuanguka ulianza upepo mkali ulioutikisa.Pia inaelezwa dalili za kuanguka kwa Mbuyu huo ulianza tangu jana mchana baada ya kupiga radi ya mvua.

Baada ya radi hiyo waliabini mzizi wa Mbuyu huo kukatika na matokeo yake ukawa umeelemewa na hivyo ilipofika leo tisa Alasiri ndipo ukaanguka.

Wakizungumza zaidi kuhusu kuanguka kwa Mbuyu huyo baadhi ya mashuhuda hao ambao hawakuwa tayari kutaja majina yao wamedai walishtuka baada ya kusikia kishindo kikubwa kumbe ndio muda ambao ulikuwa unaanguka na kusababisha mlipuko mkubwa wa umeme kutoka kukatika kwa nyaza za umeme zinazopita eneo hilo.

"Tunashukuru Mungu maana licha ya ukubwa wa mbuyu huu wakati unaanguka hakukua na mtu yoyote aliyekuwa anapita barabarani eneo hilo bali kuna gari moja ndogo ndiyo ilikuwa inapita lakini hata hivyo baada ya kupita eneo hilo ndipo mbuyu ukaanguka.


"Hivyo hakuna madhara yoyote ambayo yametokea zaidi ya kukatika umeme na uzio wa ukuta wa Ocean Road,"amesema mmoja wa mashuhuda wakati anaielezea Michuzi Blogu ambayo waandishi wake walifika kushuhudia kuanguka kwa mti huo unaodaiwa kuishi miaka zaidi ya 100.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad