HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Wednesday, 14 March 2018

MENEJA MPYA PARK HYATT ZANZIBAR KUSHIRIKI KUINUA VIPAJI VYA VIJANA 

Meneja mpya wa Park Hyatt Zanzibar Nicolas Cedro akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutambulishwa na akielezea mikakati yake ya kuinua vipaji vya vijana katika masuala ya upishi na hoteli Visiwani humo. Kushoto ni Meneja Masoko Milvas Burnice.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
UONGOZI wa Hotel ya Hyatt umemtambulisha meneja mpya wa Hoteli ya Park Hyatt Zanzibar  Nicolas Cedro ambaye amejizatiti katika kusaidia kuinua vipaji vya vijana hususani katika masuala ya upishi na hoteli.

Hoteli hiyo iliyopo maeneo maarufu ya Stone Town tayari imeshaweza kusaidia huduma za kijamii kama kufungua vituo viwili vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu, kituo cha kulea wazee wasiojiweza, elimu, maji na michezo hususani mpira wa miguu.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya utambulisho huo, Nicolas Credo amesema kuwa mbali na kuwasaidia vijana katika masuala ya hoteli ambapo tayari ameshafanya mazungumzo na Waziri wa Utalii Zanzibar Mahmoud Kombo kwa ajili ya kuweza kusaidia vijana ambapo kiutalaamu yeye ana Shahada mbili za masuala ya vyakula na uendeshaji hoteli kutoka chuo kikuu cha hoteli kilichopo Nice nchini Ufaransa pia Shahada ya uzamili ya uendeshaji wa hoteli kutoka katika chuo kikuu cha E Cornel. 

Cedro amesema kuwa atatumia uzoefu wa elimu, ujuzi wa lugha pamoja na ubunifu katika kujenga sifa na ubora wa hoteli hiyo na pia kwa wafanyakazi wake kwani akiwa kijana wa miaka 17 aliweza kuanza kuanza kazi ya upishi na pia anatambua umuhimu wa kuibua na kulea vipaji vya vijana na hivyo anategemea kushiriki katika shughuli za kijamii akiwa Zanzibar kwa kushirikiana na shule mbali mbali za kisiwani hapo za mapishi ili kusaidia vijana wenye vipaji vya upishi waweze kupata ujuzi wa kimataifa alio nao na hivyo waweze kujiendeleza katika fani hiyo na kuitumia kama njia ya kujiinua kiuchumi.

Amesema akiwa kama Meneja wa hoteli ya Park Hyatt Zanzibar na Cedro na timu yake kwa pamoja wana lengo kuu la kuipandisha hoteli hiyo kuwa katika viwango vya juu zaidi na hivyo kuchangia katika juhudi za taifa za kuhamasisha utalii nchini ikiwemo kisiwani humo kwa kushirikiana na hoteli zilizopo Italy na Ufaransa.

“Napenda kufanya kazi katika bara la Afrika na hasa katika kisiwa cha Zanzibar. Ni mahali ambapo kuna mazingira mazuri na watu wenye upendo. Nimeshafanya kazi Tanzania kwa zaidi ya miaka mitatu sasa katika hoteli ya Hyatt Regency – Kilimanjaro, Melia Zanzibar na sasa hapa Park Hyatt Zanzibar. Nimesikia furaha kubwa sana kupata nafasi hii ya kuendesha hoteli hii na nategemea kutumia ujuzi na uzoefu wangu ili kuleta ladha ya kipekee katika chakula na pia huduma tutakazowapatia wateja wetu,” alisema Cedro.

Naye Meneja wa Masoko wa Park Hyatt Zanzibar  Milvas Burnice amesema kuwa ujio wa Cedro utakuja kuwa na manufaa sana kwani ni moja kati ya watu ambao wameshafanya kazi katika hotel za Hyatt ana ana ubunifu wa hali ya juu ukiachilia mbali baadhi ya vitu ambavyo mmiliki wa hotel hizo anataka vifanywe. 
Baada ya kumaliza kaz leo narejea hom kulea. Namsubir mtt atoke shule sa 10 kwahy kaz yang ndo hyo na nyingne natuma pia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad