HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 9 March 2018

MBUNGE HAWA MCHAFU AWAASA WANAJAMII KUJIEPUSHA NA VITENDO VIOVUhab


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoani Pwani  Hawa Mchafu amewataka wanajamii wote kudumisha amani na kujiepusha na vitendo viovu ikiwa ni pamoja na uhalifu, ubakaji, matumizi ya madawa ya  kulevya, pombe haramu maarufu kama virobo na gongo,ukatili na ukandamizaji wa makundi mbalimbali katika jamii kama vile watoto, wanawake, wazee na wenye ulemavu.

Mchafu alisema hayo wakati wa  siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hapo jana yaliyofanyika katika kata ya Nyamato wilayani Mkuranga.
Mchafu aliongeza kwamba pamoja na unyanyasaji juhudi mbalimbali za wadau na serikali katika nchi yetu bado ukatili na unyanyasaji kwa wanawake ni mkubwa mno.”Katika wilaya yetu ya Mkuranga bado vitendo hivi vinaendelea katika baadhi ya maeneo ya kata na vijiji vyetu”. Mchafu alisema

Mchafu aliendelea kusema kwamba tayari serikali imechukua hatua mbalimbali ili kuondoa tofauti za kijinsia kwa kuingiza mitazamo ya kijinsia katika sera zinazowabagua wanawake “Nitumie fursa hii kuwaasa wanawake kujitokeza kushiriki katika fursa na nafasi mbalimbali na kufanya kazi kwa juhudi,maarifa na weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Tanzania ya Viwanda.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya  ya Mkuranga bwana Peter Nambunga  alisema Halmashauri kupitia  idara ya maendeleo ya jamii imeendelea kuwawezesha wanawake  kiuchumi kupitia Mfuko wa maendeleo ya wanawake na vijana kwa kutoa mikopo yenye  riba nafuu ambapo kwa miaka mitatu jumla ya fedha 366,284,500 kwa vikundi 207, vikundi vya vijana 115 na wanawake 92,vyenye jumla ya wanufaika 3075 ambapo kati yao wanawake 1,959 na wanaume 1,116.

2018/2019 Halmashauri imetenga jumla ya shilingi  cha Tshs 373, 725.040 kutoka kwenye mapato yake ya ndani kwa ajili ya kutoa  mikopo na inatarajiwa jumla ya  wanufaika  wanaokadiriwa 756 wanaume na 278 wanawake watanufaika na mikopo hiyo.

Bwana Nambunga aliendelea kusema Halmashauri imefanikisha uundwaji wa majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi ngazi ya kata na vijiji, Aidha majukwaa hayo yameundwa katika kata zote 25 na vijiji 122 na lengo la uundaji wa majukwaa hayo ni kuondoa matabaka na ubaguzi wa kiuchumi kwa wanawake ili kuleta maendeleo ya usawa.

Kwa upande wake Mwenyekiti Wa jukwaa la wanawake Mkuranga Mariamu Ulega amewaasa wanawake kuacha kujibweteka na badala yake wafuatea kauli ya Rais magufuli ya hapa Kazi tu kwa kufanya Kazi na kupeleka watoto wao shule.

Siku ya wanawake Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 machi ya kila mwaka ambapo maadhimisho haya  husisitiza na kujenga mshikamano kwa wanawake wote duniani, kuhamasisha jamii kutafakari kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake.Maadhimisho haya hutoa fursa kwa wanajamii, serikali,wananchi, wadau na wanawake wenyewe kupima utekelezaji wa maazimio, matamanio na mikataba ya kimataifa na kitaifa kuhusu masuala ya maendeleo ya wanawake na usawa wa kijinsia.

Maadhimisho haya kwa mwaka 2018 yalienda na kauli mbiu isemayo “kuelekea uchumi wa viwanda,tuimarishe usawa wa jinsia na uwezeshaji wanawake vijijini”.
 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea zawadi ya keki kutoka kwa Jukwaa la Wanawake Wila
ya ya Mkuranga.

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea na kusoma mabango ya akina mama wa wilaya hiyo katika maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake duniani yaliyofanyika Jana.
Mbunge Wa Viti Maalum Hawa Mchafu akitembelea maonesho yaliyoandaliwa na wakina mama wa Mkuranga wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Wanawake duniani Jana.

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wilaya ya Mkuranga na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani.
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu akipokea mche wa Mkorosho baada ya kuzindua kitalu hicho katika maadhimisho ya kilele cha siku ya wanawake duniani jana. Kulia ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Wilaya ya Mkuranga Mariam Ulega.Picha na Emanuel Massaka.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad