HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 20 March 2018

MASHINDANO YA 'CASTLE LAGER 5s' YAANZA KUTIMUA VUMBI JIJINI DAR

Mchezaji wa team Z,ya Ilala akijaribu kuwatoka wachezaji wa team Kiba wakati wa Bonanza la Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara Tabata mwishoni mwa wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
Mchezaji wa team Kiba,ya Ilala akijaribu kuwatoka wachezaji wa team Simba wakati wa Bonanza la Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara Tabata mwishoni mwa wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.

Mchezaji wa timu Kiba,ya Ilala akijaribu kufunga wakati wa mechi ya Bonanza dhidi ya timu Simba wakati wa Bonanza la Castle 5s(5-aside) lililofanyika Viwanja vya Sigara Tabata mwishoni mwa wiki.Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
Wachezaji wa timu ya Kenge Bar ya Kimara wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja vya Kinesi Sinza Shekilango mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
Wachezaji wa timu Ushindi ya Ubungo wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja vya Kinesi Sinza Shekilango mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.
Wawakilishi wa timu za Kinondoni wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia robo fainali wakati wa Bonanza la Castle Africa 5s(5- aside) lililofanyika Viwanja vya Jeshini Kunduchi mwishoni mwa wiki. Bingwa katika mashindano hayo ataiwakilisha inchi ya Tanzania katika mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyka Zambia.

Mashindano ya soka ya "Castle Lager Africa 5s' yalifanikiwa kuanza rasmi mwishoni mwa wiki ambapo timu 24 kutoka bar tofauti zimefanikiwa kuingia robo fainali jijini Dar es Salaam. Mashindano hayo yalichezwa katika mfumo wa bonanza yaliandaliwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia Bia yake ya Castle Lager. Kila timu itaundwa na wachezaji watano (5) na mmoja wa akiba.

Ili kupata timu shiriki, wateja wanatakiwa kununua bia ya Castle Lager kupitia katika promosheni mbalimbali zinazofanyika kwa nyakati tofauti katika baa 160 za maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam. Kuna maeneo 10 tofauti na kila eneo lina baa 16. Mteja kutoka baa husika, atatakiwa kununua bia ya Castle Lager na baadaye kupewa fomu maalumu ya kujaza ili kupendekeza majina ya wachezaji watano na mmoja wa akiba, na hakuna kiingilio au malipo yoyote kwa timu kujisajili na kushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa, baada ya kupata timu katika mchakato wa awali, kutakuwa na hatua nyingine ya upigaji wa kura kwa wateja wa baa husika, ili kupata timu moja itakayowakilisha baa hiyo.

"Baada ya kupata timu zitakazokuwa zimefanikiwa kuwakilisha baa husika, kutakuwa na bonanza maalumu ambapo timu 16 zitatoa timu nane (8) na baadaye kupata timu moja itakayowakilisha kundi moja. Timu 10 zilizopatikana katika makundi zitacheza katika bonanza kubwa litakalofanyika Aprili 28, 2018 katika Viwanja vya Leaders, jijini Dar es Salaaam," alisema Kikuli Pamoja na soka, Kikuli alisema kuwa, kutakuwa burudani ya muziki kutoka kwa wasanii mbalimbali maarufu pamoja na nyama choma na kuwa, michuano hii haitowahusisha wachezaji wanaoshiriki katika ligi zozote za nje wala ndani.

Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania katika michuano ya Afrika itakayofanyika Zambia. Endapo Tanzania itashinda katika michuano hiyo, itapata fursa ya kwenda Urusi kushuhudia mechi mojawapo ya Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, ikiambatana na mashabiki wawili watakaopatikana kwa kuchezesha bahati nasibu ya wanywaji wa Castle Lager. Katika hatua nyingine, Kikuli alimtaja mkongwe wa soka nchini, Ivo Mapunda kama balozi wa michuano hii ambaye atahudhuria mabonanza hayo kwa nyakati tofauti ili kutoa mafunzo kwa wachezaji.

Katika nyakati tofauti Mapunda aliwahi kuzichezea timu za Prisons, Simba, Yanga na Timu ya soka ya taifa 'Taifa Stars' akiwa kama mlinda mlango. Aidha ataifundisha timu ya Tanzania kabla ya kwenda Zambia, na pia endapo Tanzania itashinda ataambatana na timu hiyo kwenda Urusi kushuhudia Kombe la Dunia.

Timu za Afrika zitakashiriki katika mashindano ya Kombe la Dunia itakayoanza kutimua vumbi Juni 14 hadi 25 mwaka huu nchini Urusi ni Misri, Morocco,Tunisia, Nigeria na Senegal.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad