HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 27, 2018

MAONESHO YA WAVUMBUZI, WABUNIFU KUANZA APRILI 27 DAR


Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maonesho ya Wabunifu na Wavumbuzi, Edward Magoti(Wapili kulia) akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho hayo, leo jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola akizungumza na waandishi habari kuhusiana na maonesho ya wabunifu na wavumbuzi  yatayofanyika Aprili 27 hadi 29, leo  jijini Dar es Salaam.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
KAMATI ya Maonesho ya Wavumbuzi na Wabunifu Tanzania(TICE) kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji  wameandaa maonesho ya yayanayotarajia kufanyika kuanzia Aprili 27 hadi 29 mwaka huu katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

Akizungumza leo Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Edward Magoti amesema maonesho hayo yatahusisha Wavumbuzi na wabunifu na yatakuwa ya aina yake katika ujenzi wa sekta ya viwanda nchini.

Magoti amesema maonesho hayo ni fursa ya wabunifu na wavumbuzi katika nyanja ya kutengeneza mtandao , kujitangaza katika mtandao wa kufanya ubunifu na uvumbuzi pamoja kuendeleza kazi na uzoefu na watu wengine katika sekta hiyo.

Amesema wakati wa maonesho hayo wavumbuzi na wabunifu wa nchini Tanzania watapa fursa ya kukutana na mabalozi wa nchi mbalimbali ,wafanyabiashara wakubwa na kati taasisi za Serikali , Taasisi za fedha na viongozi.

Aidha amesema washiriki watatu kwenye maonesho hayo watapata zawadi ya milioni  Sh.35 kwa mshindi wa kwanza na mshindi mshidni wa tatu Sh.milioni 5.

Kwa upande wa Ofisa wa Habari wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Edward Nkomola amesema maonesho hayo yatakutanisha watoa huduma wote ambapo ni fursa kwa wabunifu na wavumbuzi kukutana na watoa huduma hao.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad