Mtaa Kwa Mtaa Blog

LUKUVI AELEZA MABORESHO YALIYOFANYIKA KATIKA SEKTA YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi ametaja maboresho kadhaa yaliyofanyika katika Wizara ya Ardhi.
Mhe. Lukuvi aliyasema hayo alipokutana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Akieleza Maendeleo yanayofanyika sasa katika eneo la Urasimishaji; Mhe Lukuvi alieleza kuwa zoezi la Urasimishaji sasa linaendelea kwa kasi, na kutolea mfano wa Jiji la Mwanza kuwa zoezi hilo linafanyika kwa mafanikio makubwa. Alisema; “Mpaka sasa viwanja 35,000 vimeshapimwa na Hati 12,000 kutolewa  katika wilaya za Ilemela na Nyamagana.  
Mhe. Lukuvi alisema baadhi ya maeneo mengine ambayo yamefanya zoezi la Urasimishaji kwa kiwango cha kuridhisha ni pamoja na Kimara na Makongo ambapo Wananchi wenyewe wamekuwa wahusika wakuu katika kuhakikisha kuwa wamezingatia miongozo waliopewa na Wizara kufanikisha zoezi hilo, ikiwepo kuzingatia kuainisha miundombinu muhimu kama  njia za barabara, maji , umeme n.k.
Akiendelea kufafanua jinsi eneo la Upimaji wa viwanja lilivyoboreshwa. Mhe. Waziri ameeleza kuwa sasa kuna kampuni 48 za upimaji ambazo zimesajiliwa na kuidhinishwa na Wizara, na zinazoendelea  sasa na kufanya upimaji wa viwanja katika maeneo mbalimbali nchini. 
Aidha, Mhe . Lukuvi ameeleza kuwa katika maeneo ya Vijijini pia kasi ya  upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi imekuwa ya kuridhisha, tofauti na miaka ya zamani.  Hatahivyo alieleza kuwa changamoto zipo, hususani katika mkoa wa Morogoro; katika maeneo ya Mvomero, Kilombero na mengineyo lakini Serikali inaendelea na jitihada za kufanya taratibu za upangaji wa Matumizi bora ya Ardhi na kufanya upimaji wa maeneo kwa kasi kubwa zaidi katika maeneo hayo.  
Vile vile Mhe. Lukuvi amesema katika kuboresha ulinzi wa Hati za Ardhi; Hati sasa zipo katika taratibu za kuandaliwa na kutolewa Kielektroniki. Alisema, Hati hizo za Kielektroniki zitathibiti mianya yote ya ulaghai  na rushwa, matendo ambayo yamekuwa yakifanywa kwa muda mrefu na matapeli mbalimbali na kusababisha vilio kwa Wananchi wengi.  Pia kwa Mfumo huo wa Kielektroniki kila Mmiliki wa Ardhi, atalazimika kuwajibika ipasavyo katika kulipa Kodi ya Pango la Ardhi. 
Naye Mzee Butiku amempongeza Mhe. Lukuvi katika juhudi zake za kuendelea kuboresha huduma zinazofanywa na Wizara hiyo na kumsihi kuendelea na jitihada hizo. Alisema; “Nikilinganisha hali iliyokuwepo Wizarani nyakati za nyuma na sasa, maboresho ni makubwa, endelea na juhudi unazozifanya”. 
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha muonekano wa Hati ya Kielektroniki inavyotarajiwa kuwa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere; Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
 Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akionyesha moja ya ramani za Mipango Miji kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku alipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya kazi, Mhe. William Lukuvi akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwl. Nyerere, Mzee Joseph Butiku na msaidizi wake walipofika ofisini kwake leo, katika kanda ya ofisi ya Ardhi - Dar es Salaam.
Labels:

Post a Comment

good day, to all the fantastic guys in Doha . i am new in Escorts in Doha and just arrived from Indian . i'm an Asian splendor with lovely exceptional appears, and slim and slim frame, and remarkable, sexy boobs and Lips. Doha Escorts prepared for all your offerings at my place in Heights or at your resort for a comfy night collectively. i am geared up for all forms of oral services and i am exceedingly experienced on this.

KAMERA YA MTAA KWA MTAA

[KAMERA YA MTAA KWA MTAA][carousel2]

HABARI

[HABARI][fbig1]

SHEREHE

[HARUSI][gallery1]

MKCT

Contact Form

Name

Email *

Message *

Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget