HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 27, 2018

KINARA WA UDHALILISHAJI WANAWAKE MKOANI MOROGORO AKAMATWA

Na John Nditi, Morogoro
POLISI mkoani Morogoro imefanikiwa kumnasa mtuhumiwa sugu  ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ mkazi wa Kata ya Mji Mpya , ,Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kisha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu .

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro,  Ulrich Matei alisema hayo  kwa waandishi wa habari kuhusu mkakati wa Jeshi la Polisi mkoani humo kudhibiti matukio ya uharifu na uharifu.

Alisema , kufuatia matukio kadhaa ya ukatili wa aina hiyo yaliyolipotiwa Kituo kikuu cha Polisi ndipo timu ya makachero ikiongozwa na wataalamu wa Cyber – Crime pamoja na kikosi cha kupambana na ujambazi walifuatilia suala hilo kicha kufanikisha ukamataji huo.

“ Matukio matano ya wanawake kufanyiwa vitendo vya ukatili yameripitiwa  kituo kikuu cha Polisi na wahusika wameshindwa kumtambua mihusika  na baada ya kumkamata inaimani watu wanajitokeza “ alisema Matei.

Hata hivyo alisema , baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo  alieleza mbinu anazotumia kwamba hijifanya yenye ni akari Polisi ambapo huwakamata wanawake nyakati za usiku na kuwasingizia makosa mbalimbali kasha kuwapeleka mafichoni kwenye kiza kinene maneo ya Tumbaku – Pepsi kuwatishia silaha panga , kupora mali walizonazo na kuwafanyia ukatili wa kuwalawiti na kuwapinga picha za utupu.

Alisema , mtuhumiwa baada ya kunyanya ukatili huo huchukua namba zao za simu kasha kuwapingia kwa nyakati tofauti huku akihitaji atumiwe fedha vinginevyo hutishia kuzisambaza picha zao za utupu mitandaoni.

Aidha katika mahojiano na Polisi , mtuhumiwa huyo alimtaja mtu mwingine Ramadhani Salum (35) kwa jina maaarufu ‘ Miondoko , mkazi wa Mtawala , Manispaa ya Morogoro , kuwa yenye ndiye mnunuzi wa simu zote anazopora ambaye pia amekamatwa akiwa na simu zipatazo tatu aina ya (Smart – Phone ) aina ya Tecno.

Kwa mujibu wa kamanda wa Polisi wa mkoa , alitoa wito kwa wananchi wote waliotendewa vitendo hivyo kujitokeza kiasha kuripoti kituoni ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa huyo za kufikishwa mahakamani.

Alisema kuwa, waliofanyiwa vitendo hivyo wanaweza kuja Ofisini kwake kumwona  ili kuopata ushahidi wa kutosha na kwamba picha zilizopogwa na mtuhumiwa huyo zitawasilishwa mahakamani kama ushahidi.

 Akihojiwa na waandishi wa habari mbele ya Kamanda wa Polisi wa mkoa, mtuhumiwa Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ alidai  tangu kuanza vitendo ni  wanawake watatu aliwafanyia vitendo hivyo nyakati za usiku maaneo ya  barabara ya Pepsi na Tumbaku na  hajawahi kusambaza picha hizo  mtandaoni licha ya kuwapiga.


Hata hivyo alidai kuwa, aliamua kufanya hivyo ili kupata fedha kutoka kwao  baada ya  kuwatishia kuwa endapo hawata mtumia  atazisambaza  kwenye mitandao ya kijamii  ingawa wanawake hao hawajawahi kumtumia fedha hizo.

Katika tukio jingine Polisi mkoani humo inawashikilia watu  wanne  kutokana na kufanya  matukio mawili tofauti  ya uharifu , kati ya hao watatu kuwa ni vinara wa matukio ya utapeli  na wizi kwa njia ya mtandao.

Watuhumiwa hao watatu  wanadaiwa  kumtapeli mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kiasi cha Sh 115,000  wakimwaminisha wao ni  wafanyabiashara wa  vinyago .

Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro,  Matei  aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Maulind  Higilo ( 34) , Saimon Yusuph (33) wote hao ni wakazi wa Kata ya Mazimbu  na mwingine ni Aginiwe Mbilinyi (30) mkazi wa Kata ya Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.

Watuhumiwa hao walifanya tukio hilo Machi 20, mwaka huu majira ya saa saba mchana kwa mkumtapeli mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kiasi cha Sh 115,000 huku wakimwaminisha kuwa wanabiashara ya vinyango hivyo watumiwe kiasi hicho cha fedha ili wafanikishe kuvisafirisha toka Morogoro hadi Dar es Salaam kasha wagawane faida.

Kamanda Matei alisema , watuhumiwa hao  walikamatwa wakiwa na simu tisa aina mbalimbali , kitambulisho kimoja cha mpiga kura , laini 57 za mitandano mbalimbali pamoja na kurasa sita za kitabu cha kumbukumbu kwa wakala (Log Book ) za mtandao wa Vodacom ambazo zina namba za siku za wateja.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo ya mtuhumiwa sugu   ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ (  wapili kushoto fulana nyeusi ) mkazi wa Kata ya Mji Mpya , Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kasha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu , mwingine na ( kwanza kushoto) ni mtuhumiwa wa ununuzi wa simu za wizi,  Ramadhan Salumu A.K.A Miondoko.
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo ya mtuhumiwa sugu   ajulikanaye kwa jina la Mabula  Mabula  ( 28), maarufu ‘SIX ‘ ( kati kati fulana nyeusi ) mkazi wa Kata ya Mji Mpya , ,Manispaa ya Morogoro , ambaye anajihusisha na matukio ya kubora simu kwa njia ya pikipiki , kubaka wanawake , kuwapora mali zao  kasha kuwabaka na kuwapiga picha za utupu .
 Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei (kulia) akitoa maalezo  kwa waandishi wa habari ( hawapo pichani) juu ya watuhumiwa watatu waliopo kushoto wa wizi wa mitandao  waliokamatwa na  simu tisa aina mbalimbali pamoja na laini 57 za mitandano mbalimbali ikiwa na  kurasa sita za kitabu cha kumbukumbu kwa wakala (Log Book ) za mtandao wa Vodacom ambazo zina namba za siku za wateja. ( Picha zote na John Nditi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad