HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 2 March 2018

JUMUIYA YA WAAHMADIYYA TANZANIA YAWEZESHA MAJI WAKAZI WA MITAA YA KATA KIHONDA MAGHOROFANI, MANISPAA YA MOROGORO .

Na John Nditi, Morogoro
WANANCHI wa mitaa ya Kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro  wameondokana na adha ya kutopata uhakika maji safi na salama baada kujengwa kituo cha kuchota maji ya bomba kupitia ufadhili wa Jumuiya ya Waislamu Waahamadiyya  chini ya mradi wake wa Taasisi ya International Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E).

Mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Muslim Jama’at Tanzania, Sheikh Abid Mahmood Bhatti alisema hayo  kabla ya kukaribishwa mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  katika kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro na jirani zake .

Alisema , Jumuiya hiyo pamoja na kuwa ni taasisi ya kidini , inayo mipango mbalimbali ya kutoa huduma za kijamii zikiwemo katika sekta ya afya, elimu , umeme wa soka na maji.

“ Mradi huu  ulianzishwa mwaka jana baada ya kupitishwa na Hadharat Khalifa tul Masih  kiongozi mkuu wa Jumuiya  ya waislamu waahmadiyya duniani kupitia taasisi ya IAAAE” alisema Bhatti.

Mkuu wa Chuo alisema , jamii ya Kihonda Maghorofani  iliyopo karibu na taasisi hiyo wanaweza kuchota maji lita zisizopungua 10,000 kwa siku kwa ajili ya matumizi ya nyumbani .

“ Hapa napenda kuwaomba wananchi kwamba huduma hiii ya kijamii isitumike kwa ajili ya biashara ,  huduma hii itatolewa bure kwa wakazi wote wa bila ubaguzi wa kiitikadi wa la kidini na kutolewa kuanzia asubuhi hadi jioni ya kila siku” alisema a Bhatti.

Naye Meneja wa Ahmadiyya Printing Press , Dar es Salaam, Sheikh Basharat Ur Rahman Butt alisema kuwa mradi huo ulianza kwa kuchimbwa kisima cha kina kirefu ambacho ni mita 140 na uwezo wa kuzalisha maji lita 6,000 kwa saa moja .

Alisema  kuwa , mradi huo  wa Kihonda hadi kukamilika kwake umegharimu  kiasi cha Sh  milioni 150  pamoja na mwingine mdogo wa Msikiti wa jumuiya hiyo eneo la Masika.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe aliipongeza Jumuiya hiyo kwa kuwajali watu wanyonge kuwasongezea huduma ya mradi wa maji safi na salama  ambapo alitumia fursa hiyo kumwagiza Ofisa Mtendaji wa kata hiyi pamoja na Diwani kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri wa ulinzi wa miundombonu ya maji hayo.

Dk Kebwe alisema ,mpango wa serikali hadi kufikia mwaka 2020 huduma ya maji mijini iwe imefikia asilimia 95 ambapo kwa mkoa wa Morogoro huduma hiyo kwa mjini imefikia wastani wa asilimia 71 na kwamba mradi huo ni sehemu ya utelekezaji wa mpango wa serikali wa kufikia lengo hilo.

Nao baadhi ya wakazi wa mtaa wa Kitata , Kata ya Kihonda Maghorofani , Joyce Matemu, Winfrida Laizer pamoja na Aisha Rajabu kwa nyakati tofauti walisema  kujengwa kwa kituo cha kuchota maji bure wenye bomba kumetoa unafuu wa upatikanaji maji kila siku .

Walisema mkuwa , kwa muda mrefu wamekuwa wakipata  adha ya kusubiri mgao wa kila baada ya siku mbili unaotolewa na Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Manispaa ya Morogoro (MORUWASA).
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia ) akifungua koki ya maji wa ajili ya kujaza ndoo  mara baada ya kuzindua  mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro .
 Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib ( kulia) akimtwisha  ndoo ya maji  mkazi wa Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro,   Winifrida Laizer , mara baada ya  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( hayupo pichani)  kuzindua mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni katika kituo cha Jumuiya hiyo  eneo la Kihonda Maghorofani .
 Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( kulia )akikata utepe kuashiria  kuzindua  mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro  na ( wa kwanza kulia ) ni  Amiri na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Tanzania , Tahir Mahmood Chaudhary Sahib.
  Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen Kebwe ( wapili kulia ) akioneshwa kisima cha maji  na  mkuu wa Chuo cha Ahmadiyya Morogoro , Sheikh Abid Mohmood Bhatti ( kushoto) kabla ya  kuzindua  mradi wa maji  uliojulikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro  ambayo yanawanufaisha  wa kazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani , iliyopo Manispaa ya Morogoro.
 Baadhi ya wakazi wa mitaa ya Kihonda Maghorofani ,  Manispaa ya Morogoro  wakichota maji safi na salama ya  bomba  mara baada ya  Mkuu wa mkoa , Dk Kebwe Stephen Kebwe , kuzindua  mradi wa maji  uliojilikana kwa jina la ‘ Water For Life’  hivi karibuni eneo la  kituo cha Jumuiya ya Waislamu Waahmadiyya Morogoro.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Internatioal Association of Ahmadi Architects and Engineers (I.A.A.A.E) Akram Ahmadi Sahib ( kulia) akiwa ameongozana na mmoja wa viongozi wa Ahmadiyya Muslimu Missionaries Training Centre iliyopo kata ya Kihonda Maghorofani , Manispaa ya Morogoro wakitoa kuangalia mtambo wa kusukuma maji kwa kutumia umeme wa jua. (Picha na John Nditi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad