HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, March 23, 2018

JAYDEE ATAJA WAKALI WATAKAOSHIRIKI SHOO YAKE YA UNAWEZA

Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
MALKIA wa muziki wa Bongo fleva nchini, Judith Wambura a.k.a Lady Jaydee ametaja majina ya wasanii wengine watakaomsindikiza katika Tamasha la  Unaweza linalotarajia kufanyika Machi 31 mwaka  katika Hotel ya Golden Tulip Ostetbay.

Akizungumza na Michuzi blog Jaydee amewataja wasanii hao ni Bushoke, Nick Mbishi, Alawi Junior na Wengine wengi.

"Hii ni shoo ambayo nataka kila mtu afurahie muziki akiwa nyumbani na ladha ambazo walikuwa wamezikosa kwa muda mrefu, hivyo kupitia onesho hilo nitaka kiu yao ya kutonusikia kwa muda kidogo," amesema Jaydee

Aidha mwanamuziki huyo amesema siku hiyo kutakuwa na watu maarufu akiwamo MC Pilipili na wengine wengi.

Amesema maandalizi ya shoo hiyo yamekamilika na kwamba amejiandaa vya kutosha.

Amefafanua shoo hiyo itaanza  saa12 jioni ambapo Machozi Band watakuwa jukwaani na kumalizika  saa  sita usiku atamaliza lakini ana uhakika watakaofika watakuwa wameandika historia ya aina yake kutokana na namna alivyojiandaa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad