HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, March 31, 2018

JAKAYA KIKWETE MGENI RASMI TUZO ZA SINEMA ZETU KESHO MLIMAN CITY DAR

Msanii kutoka nchini India Preetika Rao 'Alliya' akizungumza na wanahabari pamoja na wasanii wa Bongo Movie kuelekea siku ya utoaji tuzo wa Sinema Zetu, Kushoto ni mratibu wa tuzo hizo Zamaradi Nzowa na Kulia ni Mkuu wa Vipindi wa Azam Media Fatma Mohamed.

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

RAIS mstaafu wa Serikali ya Awamu ya Tano Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye shindano la Tuzo za Sinema Zetu ambazo zimeandaliwa na Azam TV kupitia kipindi cha Sinema Zetu.

Mbali ya Rais mstaafu Kikwete kuwa mgeni rasmi kwenye utoaji wa tuzo hizo utakaofanyika kesho Mliman City jijini Dar es Salaam pia kutakuwa na watu maarufu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania huku idadi ya walioalikwa ni watu 2500.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa vipindi wa Azam Media Fatma Mohammed wakati akimtambulisha kwa vyombo vya habari mgeni mualikwa katika utoaji wa tuzo hizo Muigizaji kutokea Bollywood Preetika Rao a.k.a Alliya Abulah(Malkia wake Zein)ambaye ametokea nchini India.


Hivyo baada ya kumtambulisha Alliya ndio akaeleza kuwa mgeni rasmi atakuwa Rais mstaafu Jakaya Kikwete na kufafanua walikuwa wamekaa kimya bila kueleza nano atakuwa mgeni na leo ni siku muafaka mashabiki wa Senema Zetu na Watanzania kwa ujumla kujulishwa kuhusu mgeni rasmi.

"Wapo ambao walikuwa wanadhani mgeni rasmi ni Alliya ,mgeni rasmi ni Rais Mstaafu Jakaya Kikwete na Alliya yeye ni mgeni mualikwa .Pia kutakuwa na waalikwa wengine wengi.

*Tumewaalika watu maarufu na mashuhuri karibu wote nchini.Pia tumewalika waigizaji wa filamu za Bongo na wasanii wa muziki wa kizazi kipya akiwamo Diamond na Ommy Dimpoz na wengine wengi tu.Tunao wasanii na waigizaji kutoka nchi nyingine za Afrika," amesema.

Kuhusu tuzo hizo amesema zimegawanyika kwenye vipengele 19 na katika kipengele mshindi atapata cheti cha ushindi na fedha Sh.milioni 5 kwa kila kipengele na kufafanua kabla ya kuandaa tuzo hizo walikutana na waigizaji wa filamu na kukubaliana kiasi cha fedha ambacho kinastahili kutolewa kwa mshindi.

Ametaja baadhi ya vipengele ni Muigizaji bora wa filamu, filamu bora,Mhariri bora na kufafanua vipengele no Vinci na vinahusisha makundi mbalimbali ambayo hapo kwenye tasnia ya filamu nchini maana humo wamo na waandaaji bora wa filamu.

Amefafanua tuzo hizo ni mara ya kwanza kuzitoa wao na lengo kubwa ni kuwaunganisha waigizaji wa filamu nchini Tanzania na waigizaji wa nchi nyingine ambapo watapata nafasi ya kubadilisha naomba za simu na mawazo pia.

Ameongeza wanataka kuihakikishia jamii filamu za kibongi zipo juu na zinakubalika na kwamba wamejipanga vizuri kupitia chanel ya Sinema Zetu kufanya maboresho yenye lengo la kuendeleza filamu za Bongo.
Mkuu wa Vipindi wa Azam Media Fatuma Mohamed akizungunza  na wanahabari sambamba na wasanii wa Bongo Movie wakati wa kumtambulisha Msanii kutoka Nchini India Preetika Rao Maarufu kama Alliya ambaye atakuwa moja ya waalikwa katika tuzo za Sinema Zetu zitakazofanyika Mlimani City.

Msanii Preetika Rao 'Alliyah' kutoka tamthilia ya Beintehaa akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo Movie.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad