HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 25 March 2018

FEMINA HIP YAKABIDHI TUZO KWA WANAFUNZI KUMI WA WA SHULE ZA SEKONDARI WALIOIBUKA WASHINDI SHINDANO LA UANDISHI WA INSHA

Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya vijana, Femina Hip limetoa tuzo kwa washindi kumi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi, lililoshirikisha wanafunzi wa shule za sekondari kutoka mikoa kumi na tano nchini.

Akizungumza na wanahabari wakati wa utoaji tuzo kwa washindi, Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles amesema shindano hilo lililenga kuleta uelewa pamoja na kubaini changamoto kuhusu masuala ya hedhi wanazokabiliana nazo watoto wa kike katika jamii.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Yassin Haji kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.

Amesema wanafunzi karibu 88 walishiriki shindano hilo, ambapo wavulana walikuwa 27 na wasichana 61. Na kwamba walioibuka washindi ni wasichana 5 na wavulana 5, huku shule ya Sekondari Chang’ombe ikiongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya washindi na washiriki.

“Shindano hili lililenga kupaza sauti za changamoto za wasichana wanazokutana nazo wakiwa katika siku zao.Huu mradi ulilenga kumsaidia mtoto wa kike kuwa shuleni siku zote ambazo ana hedhi, kuhakikisha uwepo wa maji shuleni na vyoo visafi,” amesema.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akizungumza katika hafla ya utoaji tuzo kwa washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi. Kushoto ni
Kiongozi wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip ambayo iliendesha shindano hilo, Lydia Charles.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Femina Hip, Sauda Simba amesema shindano hilo limebainisha changamoto wanazopata watoto wa kike wakiwa kwenye siku zao, ikiwemo ukosefu wa taulo za kujihifadhi-Pad, na kuitaka serikali pamoja na jamii kuhakikisha watoto wa kike wanapata hedhi salama.

Kwa upande wake, Balozi wa masuala ya hedhi salama, Badru Juma ameitaka serikali na jamii kutatua changamoto wanazokutana nazo watoto wa kike hasa wa kijijini.

Washindi hao ni pamoja na Veronica Felician kutoka Kondoa Girls High School kutok Dodoma, Jemima Carlos, Yasin Said,, Humphrey Otedo wote kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe, na Latifa Salumu kutoka Shule ya Sekondari Zinga. 
Wanafunzi kutpka shule za sekondari walioshiriki katika hafla ya utoaji tuzo. Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akiwa na baadhi ya washindi wa shindano la uandishi wa insha kuhusu hedhi na wachama wa Timu ya Nguvu ya Binti kutoka Femina Hip.
Mwenyekiti wa Femina Hip, Sauda Simba akimkabidhi zawadi Mshindi wa Sindano la Uandishi wa Insha kuhusu Hedhi, Humphrey Otedo kutoka Shule ya Sekondari Chang’ombe.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad