HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 12 March 2018

DC TABORA AHIMIZA MATUMIZI YA DAWA ZA KUUWA WADUDU KWA WAKULIMA

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa maelezo ya matumizi sahihi ya dawa za kuua wadudu kwa wakulima wa pamba katika Wilaya ya Nzega. Mkuu wa Mkoa huyo alikuwa katika ziara maalumu ya kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali katika mashamba ya wakulima wa pamba katika sehemu mbalimbali Wilayani humo.
 Mshauri wa Masuala ya Kilimo kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora Modest Kaijage (mwenye shati nyeupe) akitoa kwa wakulima namna ya kuwatambua wadudu mbalimbali waharibifu wa zao la pamba katika Kijiji cha Mogwa Wilayani Nzega wakati wa  ziara maalumu ya Mkuu wa Mkoa huo kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa mbalimbali kuua wadudu katika mashamba ya wakulima katika sehemu mbalimbali Wilayani Nzega.

 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (mwenye koti la Bluu ) akitoa elimu Wilayani Nzega  juu ya matumizi ya dawa ya kuua wadudu waharibifu wa pamba aina ya Dudu -All 450EC wakati wa mwendelezo wa kampeni yake ya kuelimisha jamii juu ya matumizi sahihi ya viuawadudu.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia ) na Mkuu wa Wilaya ya Nzega Godfrey Ngupula (kushoto) wakigagua shamba la Mkulima wa pamba katika kijiji cha Chamwabo wilayani Nzega ambalo lilikuwa limeathiriwa na juu na wadudu waharibifu lakini hivi limeanza kuanza matunda mapya ya pamba(vitumba).  
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(kulia) akitoa elimu kwa wakulima wa pamba wa Kijiji cha Budushi wilayani Nzega juu ya matumizi sahihi ya aina mbalimbali ya dawa za kuua wadudu wa zao la pamba. Wengine ni Afisa Ugani Kata ya Kitangili Halima Chezue(wa pili kulia), Mtendaji wa Kijiji cha Budushi Ndimiyake Noah (wa pili kutoka kushoto) na Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Kitangili Jesca Kaaya(kushoto)
 Miongoni pamba ambayo imetunzwa vizuri na kupuliziwa dawa vizuri ya kuua wadudu waharibifu katika shamba la Mkulima wa Kijiji cha Budushi Christina Bundala kama inavyoonekana.
 Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri (kulia) akimpongeza Mkulima wa Kijiji cha Budushi Wilayani Nzega Christina Bundala (kushoto) kwa kutunza vizuri shamba lake la pamba na kuweka vitumba vingi vya pamba(matunda) wakati akiwa ziara yake ya kuendesha kampeni ya utunzaji vizuri wa mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi dawa za kuua wadudu waharibifu.
 Baadhi wa wakulima wa Kijiji cha Kitangili wakiwa wanamsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Tabora (hayupo katika picha) wakati akiwa ziara yake ya kuendesha kampeni ya utunzaji vizuri wa mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi dawa za kuua wadudu waharibifu.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akiongea na waandishi wa habari kwenye shamba la Mkulima Christina Bundala (hayupo katika picha)wa Kijiji cha Budushi wilayani Nzega wakati akiwa ziara yake ya kuendesha kampeni ya utunzaji vizuri wa mashamba ya pamba kwa kupulizia sahihi dawa za kuua wadudu waharibifu.
 Picha zote Tiganya Vincent

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad