HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 29 March 2018

CHUO KIKUU CHA WAISLAMU CHA MOROGORO KUANZISHA KAMPASI KIGAMBONI JIJINI DAR ES SALAAM KATIKA MASOMO YA USIMAMIZI WA BIASHARA.

Na John Nditi, Morogoro
UONGOZI wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) kinatarajia kujenga kampasi  tawi la Kigamboni, Jijini Dar es Salaam  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara na kwa kuanzia na udahili wa wanafunzi 5,000.

Chuo hicho  Kampasi ya  Kigamboni ni kuwezesha  kupata wataalamu wengi wa  usimamizi wa biashara watakaokidhi  mahitaji  ya soko la ajira katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki  pamoja na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC).

Makamu mkuu wa Chuo Kikuu hicho, Profesa Hamza Njozi,alisema  wakati wa uwekeji wa jiwe la msingi  kitakapojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya Kigamboni , Jijini Dar es Salaam.

Profesa Njozi alisema, tangu kuanzishwa kwa Chuo hicho Oktoba 23, 2004 chini ya Mfuko wa Taasisi ya Maendeleo ya Waislamu (MDF) na kilizinduliwa rasmi Oktoba 22, 2005 na  Rais wa Serikali ya awamu ya tatu , Benjamin William Mkapa .

Makamu Mkuu wa Chuo hicho alisema, hadi  kufikia mahafali ya kumi mwaka jana ,kimeshatoa wahitimu 5,433 wa ngazi ya Shahada, Stashahada na Astashahada  ambapo  kwa sasa kina zaidi ya wanafunzi 3,000 na uwezo wa chuo ni kuchukua wanafunzi 8,000.

Profesa Njozi  alisema , kujengwa kampasi  Tawi la Kigamboni kunatarajiwa kuongeza udahili wa wanafunzi wa ndani na n je ya nchi baada  ya uongozi wa Chuo kupata  eneo la ardhi lenye  ukubwa wa ekari 400 kwa ajili ya ujenzi huo.

Makamu Mkuu wa Chuo hicho  alisema ,kitakapo  kamilika kitakuwa cha kimataifa  na  mahitaji yote muhimu  yatakayomwezesha  mwanafunzi kusoma kwa ufanisi.

 “ ….Hiki chuo kitakuwa ni cha kipekee , tutatumia wahadhiri kutoka nchi mbalimbali Duniani  kufundisha kwa njia ya Moduli , tunataka mwanafunzi  akitoka hapa awe amekamilika kuingia kwenye soko la ajira  za ushindani wa kimataifa “ alisema Profesa Njozi.

Hata hivyo alisema ,hati miliki ya kisheria  ya eneo hilo wanazo ikiwemo  pia  michoro   ya namna ya chuo kitakavyokuwa imekamilika ikijumisha  majengo ya  kisasa ya utawala, taaluma , madarasa pamoja na ya  chakula.

Alisema ,makadirio ya haraka  ya ujenzi huo unataria kugharimu zaidi ya Sh bilioni 47 hadi kukamilika kwake  na muda muafaka utakapowadia ujenzi  wa Chuo  Kampasi ya Kigamboni utaanza.

“ Tupo mbioni  kumpata mkandarasi kwa ajili ya kukamilisha taratibu za maandalizi ya awali kabla ya kuanza ujenzi wa chuo hiki” alisema Profesa Njozi.

Profesa Njozi , alisema  licha ya Chuo Kikuu hicho bado ni kichanga , jina lake linaendelea kustawi na kuchanua , ambapo Watanzania wengi wamekiamini kutokana na ubora wa taaluma na malezi yanayotolewa Chuoni hapo.

Alisema ,kwa sasa  Chuo Kikuu  kinatoa elimu ya kumwezesha pia  mhitimu kumudu  kufanya kazi mahali popote pale  ikiwemo za kujitengemea badala ya kusubiri kazi za kuajiriwa ambazo ni chache.

Naye Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo  cha MUM (MUMSO) , Yahya Khamis alisema Chuo hicho kinatekeleza  sera ya Serikali ya awamu ya tano ya Rais , Dk John Magufuli inayohimiza Tanzania ya Viwanda.

Alisema kuwa, ujenzi wa Chuo hicho ni fursa nzuri ya kuchochjea utekelezaji wake kwa kuwapata wataalamu wa usimamizi wa biashara viwandani.

“ Naiomba Serikali iongeze nguvu ili kufanikisha ujenzi huu kwa kuwa wasomi wanaotoka hapa watakwenda kusaidia katika azma ya kuifanya Tanzania ya Viwanda “ alisema Khamis.
 Makamu mkuu wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi akipanda mti baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi yake  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II, Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Makamu mkuu wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) , Profesa Hamza Njozi ( wapili kushoto  fulana pundamilia) akibadirishana mawazo na mmoja wa viongozi wa Chuo hicho baada ya  uwekaji jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi ya Kigamboni  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi  wakiume  wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakisaidia kubeba tofari  hadi eneo la  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  ya Kigamboni  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wanafunzi wakike wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM)  wakisaidia kusogeza mfuko wa saruji kwa ajili ya uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  yake itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi  na watumishi wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakisaidiana kuchimba msingi   wa  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  ya Kigamboni  itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wanafunzi wakike wa Chuo  Kikuu  cha Waislamu cha Morogoro (MUM)  wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya  uwekaji wa jiwe la msingi la ujenzi  wa Kampasi  yake itakayo kutoa shahada mbalimbali za masomo ya usimamizi wa biashara itakayojengwa eneo la Lingato , Kata ya Kisarawe II ,Manispaa ya  Kigamboni, jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanafunzi  na watumishi wengine wa  Chuo cha Waislamu cha Morogoro (MUM) wakiwa  kwenye eneo itakapojengwa Kampasi ya Kigamboni ya Chuo  kikuu hicho.
( Picha na John Nditi).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad