HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 17 March 2018

BILIONI TANO KUKAMILISHA MRADI WA UJENZI OFISI ZA MANISPAA YA KIGAMBONI

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kigamboni inatarajia kutumia zaidi ya bilioni 5 kwaajili ya ujenzi wa makao makuu ya Manispaa yanayojengwa eneo la Gezaulole katika manispaa hiyo mpya.

Akiizungumza wakati wa ziara ya kutembelea miradi ya Manispaa hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, David Sukali kwa viongozi wa UVCCM Mkoa waliotembelea kuona hatua mradi iliyofikia mwishoni mwa wiki amesema kuwa, ujenzi upo kwenye hatua za awali ambapo Mkandarasi Tanzania Building Agency(TBA) Bridge ndiye aliyepewa tenda ya ukamilishaji wa jengo hilo.

Ameongeza kuwa jengo hilo linajengwa kwa kutumia gharama kutoka Serikali kuu na fedha za ndani za Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni, Kaimu Mkurugenzi alieleza kuwa mradi utakapokamilika unatarajiwa kuwa na manufaa kwa watumishi wote wa Manispaa ya kigamboni, wakazi wote na Wilaya jirani za Kigamboni na Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa ujumla.

Amesema kuwa mradi upo kwenye hatua za awali za utekelezaji “mobilization and site clearance” ambapo fedha zilizotumika mpaka sasa ni Tshilingi.500,000,000/=.

Mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Manispaa ya Kigamboni ulianza Januari 2018 na unatarajiwa kumalizika Agosti 2018.

Viongozi wa UVCCM Mkoa walipongeza hatua zilizofikiwa na kusisitiza Mkandarasi kufanya kazi kwa juhudi ili kukamilisha mradi kwa wakati uliopangwa ili wananchi waweze kupata huduma bora.

Akifafanua kabla ya kuanza kutembelea miradi hiyo Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukali amesema kuwa miradi hii kutimiza irani ya chama cha mapinduzi ambazo ziliahidiwa katika uchaguzi wa mwaka 2015. 

Pia manispaa ya kigamboni inamradi wa kugawa pikipiki kwa kata za manispaa ya Kigamboni ambapo kila kata itapata pikipiki tano ambazo zitakuwa kwaajili ya vijana wa kata hizo kwaajili ya kujipatia kipato tofauti na wanavyoingia mikataba wanayoingia wanapata shida kubwa katika kikidhi mahitaji ya mikataba yao. 

Miradi ya Manispaa ya Kigamboni ni pamoja na ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji, ujenzi wa barabara ya kwenda Daraja la Nyerere, ujenzi wa Ofisi za Manispaa hiyozzilizopo Gezaulole na ujenzi wa Zahanati.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukali akizungumza na umoja wa vijana wa chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na wafanyakazi wa Manispaa ya Kingamboni wakati wakielekea kwenye ukaguzi wa utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni pamoja na ofisi za Manispaa hiyo jijini Dar es Salaam.
Mchumi wa Manispaa ya Kigamboni, Maximillian Manyuka akisoma matumizi  ya utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji, ofisi za Manispaa ya Kigamboni pamoja, ujenzi wa Zahanati pamoja na ujenzi wa barabara ya kuelekea daraja la Nyerere Kigamboni jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni na baadae kueekea kukagua utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji, ujenzi wa barabara ya kuelekea Daraja la Nyerere, ujenzi wa Zahanati pamoja na ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Katibu wa vijana Mkoa wa Dar es Salaam akizungumza na wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni kabla ya kuanza kutembelea miradi ya Manispaa hiyo ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya Wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni wakimsikiliza Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam,Musa Kilakala kabla yakuanza ziara ya kuangalia utekelezaji wa miradi ya Manispaa ya Kigamboni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam  na Vijana wilaya ya Kigamboni  jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Hashim Mgandilwa akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Dar es Salaam  na Vijana Wilaya ya Kigamboni pamoja na wafanyakazi wa Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigamboni, David Sukali (Mwenye suti ya  Bluu) akitoa maelekezo  kwa vijana wa  Mkoa wa Dar es  salaam na Viongozi wa vijana wa Manispaa ya Kigamboni katika Mradi wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam
 Ujenzi ukiendelea katika Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha afya cha Kimbiji katika manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Mhandisi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji, Muhidini Bunaya Sanya akitoa maelekezo ya ukamilishaji wa ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni kwa wafanyakazi wa Manispaa hiyo pamja na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapunduzi (UVCCM) pamoja na vijana wa CCM wilaya ya Kigamboni.
 Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Vijana wa Wilaya ya Kigamboni na Wafanyakazi wa Manispaa ya Kingamboni wakitembelea Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Afya Cha Kimbiji. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam,Musa Kilakala  akisaidiana na Wajenzi wa Kituo cha Afya cha Kimbiji kutandaza nondo katika ujenzi wa kiuo hicho. 
Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukali (Kushoto) akitoa maelekezo kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam,Musa Kilakala katika Jengo la Mochwari lililopo katika Kituo cha Afya cha Kimbiji katika Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa yaa Kigamboni, David Sukaliakitoa maelekezo wa viongozi wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam mara baada ya kuwasili katika eneo la ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Viongozi wa UVCCM mkoa wa Dar Dar es Salaam na Wilaya ya Kigamboni wakiangalia picha na ramani za majengo ya Ofisi za Manispaa ya igamboni zitakavyokuwa mara baada ya kukamilika.
 Viongozi wa UVCCM mkoa wa Dar es Salaam na Wilaya ya Temeke akitembelea kwenye mradi wa ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Kigamboni jijini Dar es Salaam.
 Wakipata maelekezo ya Mradi wa ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Kigamboni.
 Msanifu Majengo, Edwin Mwangasa(Mwenye tishet Nyekundu)Akitoa maelezo jinsi Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Manispaa ya Kigamboni utakavyo kamilika pamoja na changamoto zinazomkabiri mhandisi huyo.
 Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Dar es Salaam, Musa Kilakala  akisaidiana na mafundi kuweka nondo katika ujenzi wa ofisi za Manispaa ya Kigamboni.
 
Uonekano wa Majengo ya Ofisi za Manispaa ya Kigamboni zitakapokamilika hapo baadae.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad