HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 15, 2018

BENKI YA EXIM YATOA MSAADA WA VITANDA , MAGODORO 40 HOSPITALI YA MWANYAMALA LEO

 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akikabidhi Msaada wa Vitanda 4o na Magodoro 40 kwa Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe kwaajili ya hospitali ya mwananyamala jijini Dar es Salaam ikiwa ni kusheherekea siku ya Mwanamke duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8. Benki hii imetoa vitanda na magodoro kwaajili ya wodi ya akina mama katika hospitali hiyo.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akimpongeza Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda kwa msaada waliotoa benki ya Exim vitanda 40 na Magodoro 40 kwaajili ya wodi ya akinamama wanaojifungua.Ikiwa ni Kusheherekea siku ya mwanamke ambayo hufanyika Machi nane kila Mwaka.
Mlezi mkuu (Patroni) wa hospitali ya Mwananyamala, Musa Wambura (aliyesimama)akizungumza katika hafla fupi ya benki ya Exim kukabidhi vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwanayamala jijini Dar es Salaam leo kwaajili ya wodi ya akinamama wanaojifungua.
 Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa vitanda 40 na magodoro 40 katika hospitali ya Mwananyamarla jijini Dar es Salaam leo.Katikati ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe na kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda.

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe akishukuru kwa Mkuu wa Matawi ya Benki ya Exim Tanzania, Agnes Kaganda  kwa kuiona hospitali ya Mwananyamala kwa kuwa kunahospitali nyingi"Tunashukuru Mchango wenu sana Mungu awabariki ."
kushoto ni Mkuu waMatawi ya Kanda Getrude Mbunda na Kulia ni Mkuu wa matawi ya Kanda Elizabeth Mayengo.


BENKI YA EXIM TANZANIA NA KAMPENI YAKE YA MWAKA MZIMA YA KUSAIDIA JAMII.


BENKI  ya Exim Tanzania leo imekabidhi vitanda na magodoro 40 kwa Hospitali ya rufaa Mwananyamala, jijini Dar es Salaamkwa kuwa Benki ya Exim Tanzania iliadhimisha miaka 20 ya huduma, mwezi wa Agosti mwaka jana, kwa kuzindua mradi wa mwaka mzima unaoitwa “miaka 20 ya kujali jamii” ambao Benki hiyo itawekeza katika sekta ya afya Tanzania hasa kwenye kuboresha huduma za afya zinazotolewa kwa wakina mama na wanawake.

Makabidhiano hayo yamefanyika katika hospitali ya Mwananyamala wakiongozwa na wafanyakazi wanawake wa Benki ya Exim kwenye hospitali hiyo jengo la utawala  katika hospitali hiyo ukipokelewa na Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Mwananyamala Dk. Khadija Shebe.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Matawi ya benki ya Exim, Agnes Kaganda amesema “Katika kuadhimisha sherehe za wanawake mwezi huu, Benki ya Exim inatambua mchango wa wanawake katika kujenga jamii na kwenye ukuaji wa uchumi. Msingi wa mpango wetu huu wa mwaka mzima wa kujali jamii ni kuelewa kiasi gani wanawake ni muhimu katika jamii".

Benki imejitolea kusherehekea maadhimisho ya miaka 20 kwa kusaidia wanawake kwa kuboresha huduma za uzazi katika sekta ya afya. Tunaamini kwamba tuna sehemu kubwa ya kufanya mabadiliko mazuri katika sekta mbalimbali katika jamii zetu na sisi tumejizatiti kwenye mpango huu."

Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Mwananyamala, Dk. Khadija Shebe alipongeza Exim Bank Tanzania kwa msaada wake na kuhimiza taasisi mbalimbali kutekeleza ishara ya Benki ya Exim Tanzania katika kusaidia kuboresha huduma ya afya kwa wanawake nchini. Aliongezea kwa kusema “Upungufu wa vitanda katika mahospitali ni changamoto kubwa. Msaada huu kutoka benki ya Exim wa hivi vitanda 40 na magodoro utasaidia sana katika kupunguza changamoto hii .”

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad