HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 22 February 2018

WAZIRI JAFO APANIA KUBORESHA SEKTA YA AFYA KWA WAKINAMAMA WAJAWAZITO KWA KUJENGA VITO VYA AFYA

Na Victor   Masangu, Chole  Kisarawe   
WAKINAMAMA  wajawazito katika kijiji  cha Kihare kata ya Maluwi Wilaya ya Kisarawe, Mkoani Pwani  waliokuwa wanakabiliwa na changamoto katika sekta ya afya kutokana na  ukosefu wa kutokuwa na  wodi maalumu  ya kujifungulia kwa  kwa kipindi cha  muda mrefu na kuwalazimu kutembea umbari wa kilometa 15 kufuata huduma hatimaye kilio chao kimepata mkombozi baada kukamilika kwa jengo la wazazi.

Aisha Ramadhani na Fatma Iddy ni baadhi ya wakinamama ambao walisema kwa miaka mingi wamekuwa wanateseka pindi inapofika wakati wa kujifungua kutokana na zahanati ya Kihare ambayo  walikuwa wanaitumia katika kupata huduma ya matibabu ilikuwa haina jengo la wodi ya wazazi hivyo ilikuwa inawalazimu kufunga safari ya umbari wa kilometa 15 kwa kutumia usafiri wa baiskeli,pikipiki au wakati mwingine kutembea kwa  miguu.

Walisema  kwamba hapo awali walikuwa wanapata shida kubwa wakati wa kujifungua kutokana  na kutokuwepo kwa wodi ya kujifungulia hivyo walikuwa wanachanganywa na wagonjwa wengine wa kawaida kitu hali ambayo ji hatari kwa afya zao na mtoto, hivyo wameipongeza serikali ya awamu ya tano na juhudi za Mbunge wa jimbo lao  kwa kuamua kujenga jengo hilo ambalo litakuwa ni msaada mkubwa katika utoaji wa huduma.

Kwa upande wake Mganga mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jonathan Budenu  amekiri kuwepo kwa changamoto ya wakinamama wa kijiji cha Kihare  kutembea umbari mrefu wa kilometa 15 kwa ajili ya kwenda kufuata huduma ya kujifungua katika kituo cha afya chole,ambapo kwa sasa wameanza harakati za ujenzi wa  wodi kwa kutumia  za halmashauri pamoja na michango ya wananchi.

Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi  Selemani Jafo amebaini kuwepo kwa hali hiyo wakati alipokwenda kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa wodi ya wazazi katika zahanati ya Kihare ambapo  amesema kwamba katika kukabiliana na changamoto hiyo imetenga kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vitatu vya afya.

Jafo alibainisha kuwa serikali ya awamu ya tano lengo lake kubwa ni kuhakikisha inaborsha sekta ya afya hivyo ujenzi wa vituo hivyo vya afya vitaweza   kupunguza adha ya wagonjwa hususan kwa  wakinamama wajawazito kwa wananchi wa Wilaya ya Kisarawe.

“Kwa kweli katika hili la wakinamama wajawazito wamekuwa wakipata shida kubwa sana, kwani wakti mwingine wanasumbuka ya kufuata huduma ya afya kwa kutembea umbali mrefu, hivyo tumetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 500, kwa kila ujenzi wa  kituo cha afya kimoja nah ii kwa kweli itapunguza sana adha ya wakinamama waliyokuwa wakiipata pamoja na wananchi wote kwa ujumla,”alisema Jafo.

Waziri Jafo akiwa  katika ziara yake ya kikazi  Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani ambapo ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo sekta ya elimu, miundombinu, afya maji, pamoja na kuweza kukutana na viongozi, watendaji , pamoja na kungumza na wananchi wa vijiji,vitongoiji, kata kwa lengo la kuweza kusikiliza changamoto wanazokabiliana nazo kwa lengo la kuweza kuzitatua.
 Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tamisemi, Seleman Jafo akizungumza na baadi ya viongozi na watendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi kwa ajili ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya afya, maji, barabara, pamoja na elimu pamoja na kuzungumza na wananchi.
Waziri wa nchi ofisi ya Rais  Tamisemi,  Seleman Jafo (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi ya wauguzi na madaktari wa  halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbali mbai ya maendeleo pamoja na kuzungumz na wananchi.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad