HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Saturday, 10 February 2018

TPDC YATOA SHILINGI ML 25 KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA AFYA TUNDURU

 Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera kulia akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 25 kutoka kwa  maneja mawasiliano wa Shirika la maendeleo la Petroli Nchini(TPDC), Marie Msellemu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya wilayani humo.
  Mkuu wa wilaya ya Tunduru,  Juma Homera (katikati) na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya, Chiza Malando (kulia)wakifurahia mfano wa Hundi ya shilingi milioni 25  iliyotolewa na Shirikala maendeleo ya Petroli Nchini(TPDC) kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya ambacho kinatajwa mara kitakapokamilika kitasaidia kusogeza huduma za matibabu kwa wakazi wa maeneo yanayozunguka  kituo hicho kushoto ni meneja mawasiliano wa TPDC Marie Msellemu.
 Meneja mawasiliano wa Shirika la maendeleo ya Petroli nchini(TPDC), Marie Msellemu katikati mkuu wa wilaya ya Tunduru, Juma Homera wa nne kushoto na kaimu mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru, Chiza Malando wa tatu kulia wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wakuu wa idara ya halmashauri ya wilaya ya Tunduru, mara baada ya TPDC kukabidhi mchango wa shilingi milioni 25 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha Afya Nakayaya.
Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, Juma Homera akimtembeza meneja mawasiliano wa Shirika la Petroli Nchini Marie Msellemu maeneo mbalimbali ya ujenzi wa kituo cha Afya cha Nakayaya ambacho ujenzi wake umeibuliwa na kuanzishwa na mkuu huyo wa wilaya kwa kutumia wafadhili mbalimbali. Picha na Muhidin Amri

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad