HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 1 February 2018

TBL YASEMA MFUMO WAKE WA TAARIFA UKO SALAMA

*Yapunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager

Na ripota Wetu,Globu ya jamii
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL), imetoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizozagaa mitandaoni za kudukuliwa kwa mfumo wake wa kuhifadhi taarifa zake na kusisitiza mfumo huo uko salama baada ya kujiridhisha. 

Mapema jana asubuhi kulionekana taarifa ya video kwenye mtandao wa YouTube ikioesha kuna mtu aliyekuwa amevalia kofia iliyofunika uso (Mask) ikieleza kuwa, mfumo wa kuhifadhi taarifa wa TBL umedukuliwa na hivyo kuhatarisha kuvuja kwa taarifa zake muhimu. 

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Masoko wa TBL - Afrika Mashariki, Thomas Kemphuis amesema baada ya uchunguzi wa kina kampuni hiyo imejiridhisha pasipo na shaka kuwa hakuna tukio la aina hiyo lililotokea.

"Mfumo wetu wa taarifa uko salama , nitumie nafasi hii kuwahakikishia wanahisa wetu,wadau pamoja na umma kwa ujumla kutokuwa na wasiwasi,"amefafanua.

Imeelezwa nia ya TBL kuendelea kutoa huduma bora huku Kemphuis akifafanua kampuni hiyo inachukulia kwa uzito mkubwa suala la usalama wa mifumo yake na ndiyo sababu ya kufanya uchunguzi wa haraka na wakina mara baada ya kupata taarifa za uvumi kuhusu  udukuzi. 

Mkurugenzi huyo amesema kuwa TBL itaendelea kutengeneza mifumo imara ya ulinzi wa taarifa zake ili kuepuka matukio yasiyotarajiwa kama udukuzi. 

Wakati huo huo, TBL imetangaza habari njema kwa wateja wake baada ya kutoa punguzo la bei kwa bia yake pendwa ya Castle Lite Premium Lager kutoka bei ya sasa ya shilingi elfu 2,500 hadi shilingi 2,000.

Kwa mujibu wa Kemphuis, punguzo hilo la bei ni zawadi kwa wateja wa bia hiyo kwa kuwa wateja waaminifu na zaidi kwa kuiunga mkono kampuni ya TBL kupitia bidhaa zake. 

“Kupunguza bei ya bia ya Castle Lite Premium Lager kunadhihirisha shukrani zetu kwa wateja wetu kwa kutuunga mkono kwa kipindi kirefu. TBL siku zote ipo tayari kuwasikiliza wateja wake na kuwapa kile wanachokitaka,"amebainisha. #CastleLiteHacked

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad