HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 10, 2018

RAIS MAGUFULI AMPANDISHA CHEO NA KUMTEUA MOHAMED HASSAN HAJI KUWA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 10 Februari, 2018 amempandisha cheo na kumteua Bw. Mohamed Hassan Haji kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imefafanua kuwa Mhe. Rais Magufuli amempandisha cheo Bw. Mohamed Hassan Haji kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna wa Polisi (CP), na kisha kumteua kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji amepandishwa cheo na kuteuliwa kuwa Kamishna wa Polisi Zanzibar kuanzia leo tarehe 10 Februari, 2018.

Kabla ya uteuzi huu Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji alikuwa Mhasibu Mkuu wa Polisi Zanzibar.

Kamishna wa Polisi Mohamed Hassan Haji anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna wa Polisi Hamad Omar Makame ambaye amestaafu.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
10 Februari, 2018

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad