Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko leo 22 Februari 2018 ameanza
ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe ambapo pamoja na mambo mengine
atatembelea na kukagua eneo la mgodi tarajiwa wa Bafex linalotarajiwa
kuanza uchimbaji wa Madini ya dhahabu.
Maeneo
mengine atakayotembelea ni pamoja na mgodi wa uchimbaji dhahabu wa
Shanta Gold Mine uliopo katika kata ya Saza, Wilayani Songwe ambapo
atazungumza pia na wafanyakazi wa mgodi huo.
Sambamba
na hayo pia Naibu Waziri wa Madini atazungumza na wachimbaji wadogo
kwenye mkutano ulioandaliwa Mara baada ya kutembelea maeneo ya
uchimbaji.
Mara
baada ya kuwasili katika Mkoa wa Songwe Mhe Biteko amesifu juhudi za
mbunge wa Jimbo la Songwe Mhe Philiph Mulugo kutokana na uwajibikaji
mkubwa katika kuwasemea wananchi wa jimbo hilo hususani katika
kuimarisha uchumi wa wananchi kupitia sekta ya Madini.
Alisema
kuwa mbunge huyo amekuwa mstari wa mbele katika kuwatetea wananchi wake
katika katika kuchochea shughuli za maendeleo ili kuongeza ufanisi wa
maendeleo endelevu ya mtu mmoja mmoja na jamii kwa ujumla wake.
Aidha,
Mhe Biteko alimuhakikishia Mkuu wa Wilaya ya Songwe kuwa Wizara ya
Madini Kupitia sheria mpya ya madini kutakua na Tume ya Madini ambayo
kimuundo itakua na Afisa madini wa Mkoa wa Songwe ambapo utapelekea kuwa
na Ofisi hiyo ya Madini.
Mhe
Biteko aliutaka uongozi wa Wilayani na Mkoa wa Songwe kuongeza zaidi
ushirikiano na Chama Cha Mapinduzi kwani ndicho Chama chenye dhamana ya
kuisimamia na kuikosoa serikali pindi inapoenda mrama.
Alisema
kuwa baadhi ya watumishi wanapaswa kutambua kuwa wanatekeleza wajibu wa
matakwa ya ilani ya Chama Cha Mapinduzi 2015-2020 hivyo haijalishi kuwa
wanaipenda ama wanaichukia wanatakiwa kutekeleza ilani pasina kuogofya.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza mara baada ya kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Songwe kwa ajili ya ziara ya siku mbili ya kikazi katika mkoa wa Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mbele ya Kamati ya ulinzi na usalama Wilaya ya Songwe, na Kamati ya siasa ya CCM Wilaya hiyo mara baada ya kuwasili Mkoani Songwe kwa ziara ya kikazi, Leo 22 Februari 2018.
Mkuu wa wilaya ya Songwe, Mhe Samwel Jeremiah akieleza changamoto za wachimbaji wadogo katika Wilaya hiyo mbele ya Naibu Waziri wa Madini, Mhe Doto Mashaka Biteko wakati akisoma taarifa ya Mkoa wa Songwe kwa niaba ya mkuu wa Mkoa huo, Mhe Chiku Galawa, Leo 22 Februari 2018.
No comments:
Post a Comment