HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Sunday, 11 February 2018

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI MUFINDI


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa Mafinga waliojitokeza kwenye uwekaji wa jiwe la msingi la upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la upanuzi wa ujenzi wa kituo cha afya Ihongole Mafinga, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma maneno yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari ya Mgololo, Mufindi mkoani Iringa mara baada ya kulifungua ,pembeni yake ni Mwenyekiti wa Makampuni ya Rai wanaomiliki kiwanda cha Mufindi Paper Mills Bw. Jaswant S. Rai na kulia ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza. 

 ​Makamu wa  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  amesema Serikali inajitahidi kujenga na kutanua vituo vya Afya ikiwa na lengo la kupunguza msongamano kwenye hospitali za Wilaya.
Makamu wa Rais ameyasema hayo leo wakati wa kuweka jiwe la msingi  la upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole kilichopo mjini Mafinga.

Makamu wa Rais ambaye yupo kwenye ziara ya kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Iringa ambapo leo alitembele wilaya ya Mufindi na kuweka mawe ya msingi katika miradi miwili ikiwa mmoja ni wa kujenga maabara ya kisasa na madarasa na kidato cha tano na cha sita katika Sekondari ya Mgololo na upanuzi wa kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.

Akiwahutubia wananchi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa jiwe la msingi  la Upanuzi wa kituo cha Afya Ihongole , Makamu wa Rais alisema katika kila kituo cha afya kinachopanuliwa ama kujengwa Serikali imezingatia  huduma za mama na mtoto ili kupunguza vifo vya akinamama na watoto, kuborsha huduma za upasuaji .

Serikali imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa kituo hicho na kutumia mafundi wa kawaida kujenga ilikuweza kusaidia kutoa ajira kwa vijana zaidi wa eneo husika.

Makamu wa Rais amezitaka halmashauri zisimamie utoaji na matumizi ya fedha wanazotoa kwa Vijana asilimia 5 na Wanawake asilimia 5 ili kuleta tija kwenye shughuli za maendeleo.

Makamu wa Rais alisema  “tunapozungumzia uchumi wa viwanda lazima tuwaandae Vijana tangia wadogo, tuhakikishe wanafundishwa  yale yanayohitajika”.

Makamu wa Rais aliwaambia wakazi wa Mafinga, watakapokuja tena kwenye kampeni watawataka wananchi waseme Serikali yao imewafanyia nini.

Mapema leo Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ujenzi wa maabara na madarasa  ya kidato cha tano na sita katika shule ya sekondari Mgololo, ujenzi ambao utagharimu  shilingi milioni  450 za kitanzania chini ya ufadhili wa kiwanda cha Mufindi Paper Mills.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad