HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, February 6, 2018

KARANI KAMPUNI YA SGA AKWEPA KIFUNGO CHA MIAKA MITATU JELA KWA KULIPA FAINI MILIONI 100/-

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.

Mahakama ya Hakimu Mkazi  Kisutu imemuhukumu Karani wa Kampuni ya Ulinzi ya SGA, Winfred  Businge (33) kulipa faini ya Sh milioni 100 ama kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela. Baada ya kupatikana na hatia ya tuhuma za kushindwa kutolea maelzo USD  milioni moja kwa afisa forodha.

Businge ambaye ni raia wa Uganda alifanikiwa kulipa faini ya kiasi hicho cha fedha cha Sh milioni 100 na kukwepa adhabu hiyo ya kifungo.

Hukumu hiyo imesomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya mshtakiwa, kukubali kosa.

Katika hati ya mashtaka,  ilidaiwa Desemba 11, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ndani ya jiji la Dar es Salaam Businhe alikutwa ameingia nchini na USD milioni 100 ambazo ni sawa na sh. Bilioni 2  fedha ambazo alishindwa kuzitolea  maelezo kwa wakala wa forodha.

Kesi hiyo ilikuwa ikiendeshwa na Wakili wa serikali mwandamizi, Awamu Mbagwa, kwa upande wa utetezi alikuwa akiwakilishwa na Wakili Hudson Ndusyepo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad