HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, February 21, 2018

Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO akutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo

Na Koleta Njelekela, STAMICO
Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Mhandisi John Nayopa amekutana na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambaye alifika katika Ofisi za Makao Makuu ya STAMICO jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufahamiana naye na kuzungumzia namna ya kuimarisha ushirikianao katika upashanaji habari za STAMICO kwa Watanzania.
Viongozi hao walikubaliana kuimarisha ushirikiano katika suala zima la kuelimisha Watanzania kuhusu shughuli za STAMICO kwa kutumia mitandao ya kijaamii (Social Media) ya Idara ya Habari Maelezo,  Jarida la Nchi yetu linaloratibiwa na Idara hiyo na Vyombo vya Habari kwa ujumla.

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Dakta Abbasi amesema Idara yake iko tayari kutoa mafunzo kwa Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma wa STAMICO katika maeneo mbalimbali kulingana na mahitaji yao, ili kuwajengea uwezo zaidi katika taaluma zao.

“ Kulingana na ukuaji wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Idara yangu inaweza kutoa mafunzo ya kuanzia kwa wataalamu wako kuhusu Sayansi ya Mitandao ya Kijamii na uendeshaji wake; Mawasiliano kwa Umma wakati wa Majanga (Crisis Communication); pamoja na Sera na Miongozo ya matumizi ya Mitandao ya Kijamii” Alifafanua Dk. Abbasi.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Bwana Nayopa amemshukuru Dakta. Abbasi kwa kumtembelea ofisini kwake na ameahidi kuimarisha ushirikiano na Idara ya Habari Maelezo katika kuelimisha Watanzania kuhusu mchango wa STAMICO katika kuleta matokeo chanya kwenye Serikali ya awamu ya tano.
 Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Mhandisi John Nayopa akipata maelezo  kutoka kwa Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas, kuhusu majukumu ya  Idara ya Habari Maelezo na Mfumo wa Upashanaji Habari na Mawasiliano Serikalini ofisini kwake jijini Dar es Salaam .
 Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbasi (kushoto) akikabidhi Jarida la Nchi Yetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. Jarida hilo linaratibiwa na Idara ya Habari Maelezo.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Dakta Hassan Abbasi (kushoto) akitoa maelezo kwa ufupi kuhusu Jarida la Nchi Yetu toleo la Novemba 2017 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Mhandisi John Nayopa alimpomtembelea ofisni kwake jijini Dar es Salaam, hivi karibuni. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad